Kando ya UNGA, ulinzi wa amani nao kuangaziwa kwa kina

Walinda amani wakishika doria  kuwalinda raia mjini Juba,Sudan Kusini.
UNMISS
Walinda amani wakishika doria kuwalinda raia mjini Juba,Sudan Kusini.

Kando ya UNGA, ulinzi wa amani nao kuangaziwa kwa kina

Amani na Usalama

Mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukianza leo, wakuu wa nchi na viongozi wa serikali wa nchi zinazochangia kwenye operesheni za ulinzi wa amani wanakutana kujadili jinsi ya kukabiliana na changamoto za ulinzi wa amani.

Akizungumzia lengo la mkutano huo Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix amesema pamoja na kumulika kampeni ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliyoanzisha mwaka huu ya kuimarisha ulinzi wa amani kupitia hatua za pamoja, mkutano huo...

Ni kuhusu kuwaelezea  mataifa wanachama kuhusu changamoto muhimu kuhusu ulinzi wa amani, na pia kuwaeleza kuwa tunahitaji kutuunga mkono. Mkutano huu pia ni kuhusu kuihamasisha jamii ya kimataifa, wanachama wetu kuhusu ulinzi wa amani na kuzungumzia changamoto tulizo nazo katika ulinzi wa amani.”

Suala lingine ni usawa wa kijinsia katika ulinzi wa amani ambapo Bwana Lacroix anaelezea kile kinachopaswa kufanya kuondoa hali ya sasa..

"Nadhani kuna vitu vingi tunavyoweza kufanya, na ni shabaha muhimu sana kwa sababu, kukiwa na wanawake wengi katika ulinzi wa amani ina maana kuwa ulinzi unakuwa madhubuti. Kwa hiyo mosi ni kuwaomba wanachama kuwa waendelee kufanya juhudi hizo za kutupatia idadi kubwa zaidi ya walinda amani wanawake. Pili ni kuhakikisha kuwa mazingira yetu ya kazi ni sahihi kwa wanawake. Nadhani ya tatu ni kuona kama tunatoa mwanya zaidi kwa wanawake kuweza kuchagia zaidi katika ulinzi wa amani.”