Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MKUTANO WA 73 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA

MKUTANO WA 73 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
MJADALA MKUU WA UNGA73

Mkutano wa 73 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaanza mwezi huu wa Septemba hadi wiki ya pili ya mwezi Septemba mwakani. Katika ukurasa huu hata hivyo tutakuwa tunakuletea habari motomoto kutoka mjadala wa wazi na vikao vya ngazi ya juu vya mkutano huo ambavyo vinafanyika kuanzia tarehe 25 septemba 2018 hadi Oktoba mosi 2018. Pamoja na hotuba za viongozi ni vikao vya ngazi ya juu kuhusu Kifua Kikuu, Ulinzi wa Amani, tukio maalum la kumuenzi hayati Nelson Mandela na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, NCDs.

UN Photo/Mark Garten)

Naona mustakabali mkubwa ambao unaongozwa na vijana-Restless Development

Umoja wa Mataifa Jumatatu hii umezindua mkakati wake mpya kuhusu vijana ukilenga kuimarisha mchango wa takribani vijana bilioni 2 duniani  kwa lengo la  kukuza amani, uadilifu pamoja na kuwa na  dunia endelevu. Mkakati huo umepatiwa jina,  “Vijana 2030:Mkakati wa  Umoja wa Mataifa  kwa vijana,”  umeshuhudiwa  na viongozi wa nchi na wakuu wa serikali, lakini pia vijana ambapo mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo la kihistoria kutoka shirika la kiraia la Restless Development amezungumza na Grace Kaneiya wa Idhaa hii punde tu baada ya tukio hilo na anaanza kwa kujitambulisha.

Sauti
3'48"