Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Mabadiliko ya Tabianchi
Fursa ya kipekee kwa kila mtu duniani kushiriki katika kuamua mstakabali wa Ulimwengu.
Umoja wa mataifa, umetoa taarifa ya kuwataka watu wote kote duniani kwa mara ya kwanza kushiriki moja kwa moja katika mkutano muhimu wa kusaka mustakabali wa dunia kwa kutafuta namna ya kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi.
Guterres aelezea mshikamano wake na Marekani kufuatia moto jimboni California
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelezea kusikitishwa kwake kufuatia taarifa za vifo na uharibifu mkubwa kutokana na moto wa nyika unaoendelea kukumba jimbo la California nchini Marekani.
Sasa ufuta tunavuna, tunakula na tunauza shukrani IFAD- Wakulima Chad
Nchini Chad mradi wa mfumo wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD umesaidia wakulima kukabiliana na matatizo yaliyowakumba katika kilimo cha zao la ufuta linalotegemewa kwa lishe na kipato.
Ndani ya nyumba ya mkulima mmoja nchini Chad, anaonekana Pierre Thaim, balozi huyu wa mapishi ya Afrika kutoka New York, Marekani akiwa amemtembelea mkulima wa ufuta Fatime Saleh ili kujionea jinsi mabadiliko ya tabianchi yaliyoathiri kilimo cha zao hili. Kwa pamoja wanasaidiana kusagisha ufuta, kiambato muhimu kwa mlo kwenye nchi hii ya Afrika Magharibi.
Kuimarika kwa tabaka la ozoni ni tija dhidi ya mabadiliko ya tabianchi-UN
Matokeo ya utafiti mpya yalitotolewa leo na ripoti ya Umoja wa Mataifa yanaonyesha kuwa kuendelea kuimarika kwa tabaka la ozoni kumechukuliwa kama mfano wa mafanikioambayo yanayoweza kufikiwa na mikataba ya kimataifa, na kama chagizo la hatua zaidi za kukomesha ongezeko la joto duniani.
Majanga ya asili yamesababisha hasara kubwa ya kiuchumi duniani :ripoti
Miaka 20 iliyopita imeshudia ongezeko la asilimia 151 ya hasara ya kiuchumi ya moja kwa moja kote duniani kutokana na majanga yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi, imesema ripoti mpya iliyotolewa na Umoja wa Mataifa .
Ripoti ya IPCC ni kengele ya kutuamsha kuhusu mabadiliko ya tabia nchi:Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo ameonya kwamba ripoti mpya ya jopo la kimataifa la Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ni kengele ya kuiamsha Dunia kuchukua hatua zaidi dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Tusipochukua hatua sasa dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi tutalipa gharama kubwa-UN
Mabadiliko ya tabia nchi yana athari na yataendelea kuwa na athari kubwa katika haki mbalimbali za binadamu ikiwemo haki ya kuishi, afya, chakula na maji lakini pia haki ya kuwa na mazingira bora endapo hatua madhubuti hazitochukuliwa.
Mazao yaliyotelekezwa sasa kugeuka mkombozi wa njaa:FAO
Katika historia ya mwandamu, kati ya aina 30,000 za mimea , ni aina 6000 hadi 7000 pekee ndizo zimekuwa zikilimwa kwa ajili ya chakula kufikia leo hii , na ni takriban aina 170 tu za mazao ndio zinatumika kwa kiwango kikubwa katika biashara , kwa mujibu wa ripoti ya shirika la chakula na kilimo FAO iliyotolewa juma hili.
Si hiyari, ni lazima kulikabili jinamizi la mabadiliko ya tabia nchi:Guterres
Mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 73 umefunguliwa rasmi hii leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Wawakilishi kutoka nchi 193 wanachama, mashirika ya kimataifa, asasi za kiraia na wadau wengine wa maendeleo wakikutana kwa lengo la kuhakikisha ajenda ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa inatimia ifikapo 2030.
Viwango vya joto duniani ni vya juu tuchukue hatua zaidi kudhibiti- Guterres
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuhifadhi tabaka la ozoni, Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amesema mwaka huu umevunja rekodi ya joto kali duniani kote na pia kuwa ni wakati muhimu kuchukua hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.