Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majanga ya asili yamesababisha hasara kubwa ya kiuchumi duniani :ripoti

Tarehe 30 Septemba 2018 nchini Indonesia , magari na nyumba zilizosambaratishwa na tetemeko Balaroa National Park katikati mwa jimbo la Sulawesi
© UNICEF/Arimacs Wilander
Tarehe 30 Septemba 2018 nchini Indonesia , magari na nyumba zilizosambaratishwa na tetemeko Balaroa National Park katikati mwa jimbo la Sulawesi

Majanga ya asili yamesababisha hasara kubwa ya kiuchumi duniani :ripoti

Tabianchi na mazingira

Miaka 20 iliyopita imeshudia  ongezeko la asilimia 151 ya hasara ya kiuchumi ya moja kwa moja  kote duniani kutokana na majanga yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi, imesema ripoti mpya iliyotolewa na Umoja wa Mataifa .

Ripoti h ambayo imetolewa leo mjini Geneva Uswisi na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na  kupunguza kwa hatari za majanga,UNISDR inasema kuwa mataifa ambayo yalikabiliwa na majanga katika kipindi kati ya mwaka wa 1998 hadi 2017, yaliarifu hasara ya moja kwa moja ya kiuchumi ya dola bilioni 2,908 ambapo majanga yanayohusiana na  tabianchi gharama yake ilikuwa  dola bilioni 2,245 ambazo ni sawa na asilimia 77.

Akigusia ripoti hii, katika mkutano na waandishi habari mjini Geneva, Ricardo Mena, mkuu wa kitengo kinachochunguza na kusaidia utekelezaji katika shirika la UNISDR amesema kuwa, kawaida wanaoathirika mno na majanga ni kutoka katika maeneo masikini mno.

(SAUTI YA RICARDO MENA)

“ Lakini la ajabu ni kuwa ripoti inaonyesha kama   kutokana na kutokuwa salama, watu katika mataifa ya kipato cha chini na cha wastani wananafasi ya mara saba kuweza kuawa na majanga kuliko wale waishio katika mataifa ambayo yamendelea.Kwa hivyo hii inatilia mkazo haja ya kuhakikisha kuwa tunadhibiti utoaji wa hewa chafuzi ili hali isiharibike na pia haja ya kuwekeza katika hatua za kupunguza majanga.”

 

Mtu akitembea na kuona gari linaloning'inia kwenye paa ya nyumba baada ya tetemeko la ardhi na tsunami Palu katikati ya Sulawesi Inonesia 29 Septemba 2018
© UNICEF/Arimacs Wilander
Mtu akitembea na kuona gari linaloning'inia kwenye paa ya nyumba baada ya tetemeko la ardhi na tsunami Palu katikati ya Sulawesi Inonesia 29 Septemba 2018

Hata hivyo hasara ya kiuchumi imekumba zaidi mataifa yaliyoendelea ambapo katika orodha Marekani inaoongozwa kwa kupata hasara ya zaidi ya dola bilioni 944 huku China dola bilioni 492.

Katika kipindi hicho cha miaka 20 zaidi ya watu milioni 1 walipoteza maisha yao na bilioni 4.4 walijeruhiwa, kupoteza makazi yao, au walihitaji msaada wa dharura.

Mkuu wa UNISDR Mami Mizutori, amesema uchanganuzi wa ripoti hiyo unaonyesha matukio ya hali mbaya ya hewa ni kizuizi katika vita dhidi ya umaskini katika maeneo kunatokea sana majanga.

Ripoti hii inayoonyesha kuwa hasara ya kipindi hiki ni ya juu ikilinganishwa na ya kipindi cha nyuma, imetolewa kuelekea siku ya kimataifa ya kupunguza majanga tarehe 13 mwezi Oktoba