Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

UN Photo/Sophia Paris

Taka zaepusha matumizi ya dizeli Uganda

Matumizi ya nishati mbadala na salama ni jambo ambalo linapigiwa chepuo na Umoja wa Mataifa ambapo lengo namba 7 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linasisitiza nishati rahisi na salama. Hatua hii inazingatia kwamba idadi ya watu wanaohitaji nishati ya umeme inaongezeka kila siku na hivyo kutoa changamoto ya kusaka vyanzo mbadala vya nishati kwani umeme pekee uliozoeleka ni wa vyanzo vya maji, na ukame unatishia uwepo wa mabwawa ya maji. Ni kwa kuzingatia hilo huko Uganda, wanatumia mabaki ya taka au biomasi ili kuzalisha nishati. Je nini kinafanyika?

Sauti
3'16"

Mwaka mmoja wa mkataba wa Paris, mafanikio ni dhahiri

Mkutano wenye lengo la kuchagiza utekelezaji wa mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi utafanyika kesho mjini Paris, Ufaransa, ukienda sambamba na maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kutiwa saini kwa nyaraka hiyo.

Viongozi wa ngazi ya juu watashiriki mkutano huo akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres, Rais wa benki ya Dunia pamoja na mwenyeji wao Rais wa Ufaransa.

Wakati wa mkutano huo, hatua zinazochukuliwa za kufanikisha mkataba huo zitawekwa bayana ikiwemo hatua za nchi kukabili mabadiliko ya tabianchi.

Uhakika wa chakula na lishe ni changamoto kubwa Asia na Ulaya:FAO

Baadhi ya nchi za Ulaya na Asia ya Kati ni miongoni mwa nchi ambazo zimeathirika zaidi na  mabadiliko ya tabianchi, hali ambayo imesababisha uharibifu wa mazao, misitu na pia kuathiri sekta ya ufugaji na uvuvi.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya iliyozinduliwa leo na shirika la chakula na kilimo duniani, FAO yenye kichwa “Kuhakikisha uhakika wa chakula kupitia njia bora za usimamizi wa rasilimali za asili kwa kuzingatia mabadiliko ya tabianchi”.

Saidieni kupambana na uharibifu wa mazingira: Guterres

Tuna haki ya kuishi sehemu salama, tunategemea kula chakula bora, maji safi na kuvuta hewa safi lakini bado tunaendelea kuharibu mazingira.

Huo ni ujumbe wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika mkutano mkuu wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa unaofanyika Nairobi, Kenya.

Guterres amesema tayari kuna mbinu na maazimio madhubuti za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi yanayoweza kuigwa kuinusuru dunia isiendelee kuathirika.