Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sasa ufuta tunavuna, tunakula na tunauza shukrani IFAD- Wakulima Chad

Sasa ufuta tunavuna, tunakula na tunauza shukrani IFAD- Wakulima Chad

Pakua

Nchini Chad mradi wa mfumo wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD umesaidia wakulima kukabiliana na matatizo yaliyowakumba katika kilimo cha zao la ufuta linalotegemewa kwa lishe na kipato. 

Ndani ya nyumba ya mkulima mmoja nchini Chad, anaonekana Pierre Thaim, balozi huyu wa mapishi ya Afrika kutoka New York, Marekani akiwa amemtembelea mkulima wa ufuta Fatime Saleh ili kujionea jinsi mabadiliko ya tabianchi yaliyoathiri kilimo cha zao hili. Kwa pamoja wanasaidiana kusagisha ufuta, kiambato muhimu kwa mlo kwenye nchi hii ya Afrika Magharibi.

Kisha wanakwenda shambani ambako Fatime anafunguka..

“Nilipokuwa mtoto, misimu ya mvua ilikuwa mizuri. Mbegu za asili ambazo wazazi wangu walikuwa wanapanda, zilikomaa kwa wakati. Sasa kuna mabadiliko. Kilimo cha ufuta ni muhimu kwangu. Bila ufuta hatuwezi kufanya chochote. Nikiuza gunia moja naweza kununua sabuni, na mahitaji mengine ya shule ya wanangu.”

IFAD ilisikia kilio cha Fatime na wenzake na kutekeleza mradi ambao pamoja na kuwapatia mbegu za ufuta zinazokomaa haraka hata mvua zinazokuwa kidogo, wanafundishwa jinsi ya kupanda mazao na kuchambua taarifa za hali ya hewa.

Baada ya mafunzo, ufuta umestawi na wakulima wanaweza kuvuna ufuta katika muda mfupi, sasa wakiwa nyumbani Fatime anatumia ufuta kwa mapishi waliyozowea kama vile ugali, supu na vitamutamu na balozi wa mapishi ya kiafri Thaim anasema..

“Cha kufurahishi ni kwamba kwa kiambato kimoja tu kama ufuta, anaweza kutengeneza vitu tofauti. Anapate fedha kwa kuuza mafuta sokoni, na anaandaa mapishi mbalimbali.”

Mlo umekamilika na Fatime na familia yake pamoja na mgeni wao balozi wa mapishi Thaim wanafurahi mlo mkekani kwa pamoja wakiwa na hakikisho la lishe na kipato.

Audio Credit
Arnold Kayanda
Audio Duration
1'50"
Photo Credit
IFAD