Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Wafanyakazi wa ujenzi katika kituo cha kuzalisha umeme wa maji cha Trung Son Vietnam
World Bank/Mai Ky

Msongo utokanao na ongezeko la joto utasababisha hasara sawa na kazi milioni 80 ifikapo mwaka 2030-“ILO

Makadirio kwa kuzingatia ongezeko la joto la dunia la nyuzi joto 1.5 kufikia mwishoni mwa karne hii yanaonesha kuwa kufika mwaka 2030, asilimilia 2.2 ya jumla ya muda wa saa za kazi kote duniani itapotea kutokana na joto kali, na ni hasara sawa na nafasi za kazi milioni 80.  Maelezo zaidi na Patrick Newma

 

Sauti
2'31"
FAO

Mabadiliko ya tabianchi ni janga kwa wafugaji Uganda

Mabadiliko ya tabianchi ni janga ambalo linaikabili dunia hii leo ambapo Umoja wa Mataifa na washirika wake kupitia lengo nambari 13 la ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endeleve au SDGs, wamekuwa msatari wa mbele kubonga bongo ili  kutafuta suluhisho ikiwa ni pamoja na  kuhamisha serikali na asasi mbalimbali kuweza kutafuta njia mbadala ya kupambana na janga hili.

Sauti
3'48"
UNICEF/Mulugeta Ayene

 IFAD yawajenga mnepo wakulima nchini Ethiopia.

Zaidi ya watu bilioni moja kote duniani wanaishi katika maeneo ambayo yana uhaba mkubwa wa maji, na watu wengine wapatao bilioni 3.5 watakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa maji ifikapo mwaka 2025 kwa mujibu wa takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO na shirika la maendeleo ya kilimo IFAD.

Sauti
3'6"

24 Juni 2019

Katika Jarida la Habari hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Baraza la Haki za binadam laanza geneva kamishina Mkuu Michelle Bachelet ataka Cameroon tambueni wapinzani kama wadau wa  mchakato wa amani

-Balozi mwema mpya wa UNHCR Mercy Masika asema atatumia kipaji chake kukirimu wakimbizi Kenya na kwingineko

-Kuwasaidia wakimbizi na wenyeji wao, ni njia nzuri ya kuwahudumia watu waliotawanywa Uganda yasema Benki ya Dunia

Sauti
10'50"