Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

WFP/Photolibrary

Dkt Agnes Kijazi: Hali ya hewa haina mipaka, ni muhimu nchi zote tushirikiane.

Mkutano wa sayansi, teknolojia na ubunifu unakunja jamvi hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo wabunifu wa sayansi na wabobevu wa teknolojia wamejadiliana kwa siku mbili.  Miongoni mwao ni Dkt Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania ambaye ni mmoja wa wajumbe 10 wa jopo la ngazi ya juu la Umoja wa Mataifa la kutoa ushauri kuhusu jinsi sayansi na teknolojia inavyoweza kutumika kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Sauti
2'29"
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa antonio Guterres katika mkutano na waandishi wa habari akiwa na waziri mkuu wa New Zealand mjini Aucland
UN Photo/Mark Garten)

Heko New zealand kwa vita dhidi ya silaha, chuki, na mabadiliko ya tabianchi:UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterees yupo ziarani , Auckland, mjii mkuu wa New Zealand hii leo, ambapo kwenye mkutano wa  pamoja na Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Arden mbele ya waandishi wa habari amesisitiza ushirikiano wake na waathirika wa mashambulizi dhidi ya msikiti katika mji wa Christchurch mwezi Machi yaliyokatili maisha ya  watu 51 na kujeruhi wengi wengine.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (Kulia) na mwenyekiti wa tume ya Muungano wa Afrika Moussa Faki Mahamat wakihutubia waandishi wa habari.
Video Screen Shot

Kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, usalama na amani ni muhimu katika kufikia maendeleo Afrika-AU, UN

Mabadiliko ya tabianchi ni moja ya masuala ambayo yataathiri ukuaji wa uchumi wa bara Afrika iwapo uchafuzi wa mazingira hautapunguzwa kwa asilimia 45 kufikia mwaka 2030 na kutokomezwa kabisa ifikapo mwaka 2050 amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia waandishi wa habari Jumatatu alasiri jijini New York, Marekani.

UN News Kiswhaili/Patrick Newman

Teknolojia ya asili ya wafugaji inasaidia mnepo wa mabadiliko ya tabianchi:TANIPE

Changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa hazichagui wala hazibagui taifa au jamii utokayo zinamuathiri kila mtu duniani na ndio maana wito unatolewa kila uchao kuchukua hatua zote stahiki kujenga mnepo dhidi ya zahma hiyo kote duniani. Wito huo hivi sasa unaitikiwa sio tu na serikali mbalimbali kuweka será na mikakati , bali pia wadau wote wakiwemo asasi za kiraia ,sekta binafsi, jamii na hata mashirika ya kijamii.

Sauti
5'15"
UNEP

Wanawake Uganda, vinara wa kuwalinda Sokwe wasitoweke.

Kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo mabadiliko ya tabianchi yaliyosababisha binadamu kusogea zaidi katika makazi asili ya wanyama, mara kadhaa binadamu na wanyama wameingia katika mgogoro ambao unaziathiri pande zote mbili. Migogoro hiyo ni pamoja na wanyama kuvamia makazi ya binadamu na hata kuharibu mashamba huku binadamu nao wakisambaratisha makazi ya wanyama.

Sauti
3'44"