Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuimarika kwa tabaka la ozoni ni tija dhidi ya mabadiliko ya tabianchi-UN

Tabaka la ozoni linaendelea kuimarika.
UNEP
Tabaka la ozoni linaendelea kuimarika.

Kuimarika kwa tabaka la ozoni ni tija dhidi ya mabadiliko ya tabianchi-UN

Tabianchi na mazingira

Matokeo ya utafiti mpya yalitotolewa leo na ripoti ya Umoja wa Mataifa yanaonyesha kuwa kuendelea kuimarika kwa tabaka la ozoni kumechukuliwa kama mfano wa mafanikioambayo yanayoweza kufikiwa na mikataba ya kimataifa, na kama chagizo la hatua zaidi za kukomesha ongezeko la joto duniani. 

Matokeo ya utafiti huo ambao niUchunguzi wa kisayansi kuhusu kutoweka kwa tabaka la Ozoni 2018” ni ya karibuni kabisa katika mfululizo wa ripoti zinazotolewa kila baada ya miaka minne ambazo zinafuatilia kuimarika kwa tabaka la Ozoni, tabaka ambalo linalinda maisha ya duniani dhidi ya miale hatari ya jua.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira, UNEP na jopo la kimataifa kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabianchi IPCC, tangu kufanyika kwa tathimini ya mwisho mwaka 2014, tabaka la Ozoni linaonekana kuendelea kuimarika na uharibifu kupungua .

IPCC inasema sehemu ya tabaka la Ozoni imerekebika kwa kiwango cha asilimia 1-3 tangu mwaka 2000 katika upande ncha ya kaskazini ya dunia, na katikati mwa dunia tabaka hilo linatarajiwa kutengamaa kabisa ifikapo miaka ya 2030, ikifuatiwa na ncha ya kusini mwa dunia katika miaka ya 2050 huku ukanda wa pola mwaka 2060.

IPCC imeongeza kuwa mafanikio haya yanatokana na hatua zilizokubalika kimataifa chini ya mkataba wa Montreal ambao ulianza kutekelezwa takribani miaka 30 iliyopita kufuatia madai kwamba chembechembe za tabaka la Ozoni ambazo zilikuwa zikisaidia kuilinda dunia dhidi ya miale mikali ya jua zimeanza kutoweka na hivyo kuruhusu miale hiyo kupenyeza moja kwa moja duniani.

Image
Utafiti na uangalizi wa ozone na hali ya hewa. Picha: WMO

 

Mwakani mkataba huo umeelezwa utapatiwa nguvu zaidi kufuatia kuridhiwa kwa makubaliano ya Kigali ambayo yanatoa wito wa kupunguza matumizi ya baadaye ya gesi kwenye majokofu  na viyoyozi.

Mkataba wa Montreal ni moja ya makubaliano ya kimataifa yaliyopata mafanikio katiia historia na ni kwa sababu maalumu” amesema Mkuu wa UNEP Etik Solheim na kuongeza kuwa “Mamlaka ya kisayansi na hatua za ushirikiano ambazo zimeongoza mkataba huo kwa miaka 30 ukiwa na lengo la kukarabati tabaka la Ozoni, ndio sababu ya makubaliano ya Kigali kushikilia ufunguo wa ahadi ya hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi hapo baadaye.”

Matokeo hayo ya utafiti yanatoa mwanya wa matumaini ikiwa ni chini ya mwezi mmoja baada ya IPCC kutoa ripoti iliyoelezea hali mbaya na athari za ongezeko la joto duniani kwa nyuzi joto 2 ikilinganishwa na ilivyokuwa kabla ya maendeleo ya viwanda .

Waandishi wa ripoti hiyo wamebaini kwamba endapo makubaliano ya Kigali yatatekelezwa kikamilifu na dunia inaweza kuepuka hadi asilimia 0.4 ya ongezeko la joto duniani karne hii, ikimaanisha kwamba utakuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha ongezeko la joto duniani halizidi nyuzi joto 2.