Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushiriki wa baba mtoto anapozaliwa una faida zake

Ushiriki wa baba mtoto anapozaliwa una faida zake

Pakua

Ni kawaida barani Afrika kushuhudia mama anapotaka kujifungua kuwa hospitali peke yake, tofauti na mataifa mengi yaliyoendelea ambapo baba ana nafasi yake katika kushuhudia mwanae akizaliwa. Nchini Uganda mambo yameanza kubadilika na wanaume wametambua umuhimu wa kuwa sanjari na kina mama au wake zao wanapojifungua. Kwa undani zaidi ungana na mwandishi wetu John Kibego katika makala hii ya wanawake na uzazi nchini humo.

Photo Credit
Akina mama kwenye hospitali ya rufaa ya Hoima baada ya kijifungua. Picha: UM/John Kibego