Ubunifu wa nguo za magome ya miti na uhifadhi wa mazingira Burundi-sehemu 1
Katika Juhudi za kuunda ajira na kuhifadhi mazingira, msichana kutoka Burundi Annick Kabatesi ameanzisha mradi wa kutengeneza nguo zitokanazo na magome ya miti. Nguo hizo zimetajwa kuwa zinazingatia uhifadhi wa mazingira. Bi. Kabatesi ambaye ni mwanamitindo pia amejijengea umaarufu mkubwa kwa kutengeneza nguo hizo za magome ya miti baada ya nguo hizo kuwavutia viongozi wakuu Serikalini.
Sambamba na mpango huo wa nguo za miti, mwanaharakati huyo wa mazingira Annick Kabatesi ameanzisha pia mpango wa kupanda miche ya miti ili kurejeshea miti inayokatwa kwa shughuli hiyo ya kutengeneza nguo kwa kutumia magome ya miti. Mwandishi wetu wa Maziwa makuu Ramadhani KIBUGA amezungumza na Annick Kabatesi kuhusu mradi huo na katika sehemu hii ya kwanza anaangazia wanavyopata magome ya miti na kutengeneza kitambaa.