Tanzania yaongeza vituo vya uchunguzi wa TB ili kufikia watu wengi zaidi

Tanzania yaongeza vituo vya uchunguzi wa TB ili kufikia watu wengi zaidi

Pakua

Hii leo shirika la afya ulimwenguni WHO limetoa ripoti kuhusu hali ya ugonjwa wa Kifua Kikuu au TB duniani ambapo kuna matumaini na wakati huo huo bado kuna changamoto. Mathalani WHO inasema idadi ya vifo kutokanana TB ilipungua kwa visa 400,000 ikilinganishwa mwaka jana na miaka 16 iliyopita. Na wakati huo huo kuna changamoto ikiwemo kuwafikia wagonjwa ambao wanakosekana katika kupima na kupatiwa tiba bara la Afrika ikiwa ni miongoni. Ni kwa mantiki hiyo Assumpta Massoi amezungumza na Dkt. Liberate Meloh, Meneja Msaizidi wa mpango taifa wa Ukoma na Kifua Kikuu nchini humo,  NLTP kuhusu hali ilivyo nchini humo ambapo Dkt. Meloh anaanza kwa kuangazia Tanzania iko wapi kwenye harakati dhidi ya TB

Photo Credit
Watendaji wa mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma nchini Tanzania, NTLP wakifuatilia usimamizi wa dawa kwenye moja ya maduka ya dawa muhimu chini ya Mpango wa ADDO. Pichani mtendaji akikagua fomu anayopatiwa mgonjwa anapatiwa mtu anayehisiwa kuwa na ug