Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

UN News/Patrick Newman

Mahojiano na mbunge wa Kenya kuhusu uhamiaji

Wabunge kutoka nchi mbalimbali duniani wakiwa  makao makuu ya Umoja wa Mataifa  mjini New York Marekani kubadilisha mawazo ya jinsi ya kukabiliana na suala mtambuka la uhamiaji.

Miongoni mwa wabunge wanaoishiriki ni mbunge wa jimbo la Kiambu Kenya  Jude Njomo.Katika mazungumzo na mwanahabari wa UN Siraj Kalyango amezungumzia masuala mbalimbali kuhusu uhamiaji akianza na kwanini watu wanahama kutoka mataifa yao mama. 

Sauti
3'53"
Jane John (TBC-Tanzania)

Radio haifi ng'o

Ujumbe wa siku ya radio duniani mwaka huu wa 2018 ni Radio na Michezo! Umoja wa Mataifa unataka chombo hicho adhimu kitumike kusaidia watu kuchanua na kuonyesha uwezo wao wote. Miongoni mwa watu ambao radio imeweza kuibua stadi zao ni Jane John, mtangazaji wa kike wa habari za michezo katika shirika la utangazaji nchini Tanzania, TBC. Assumpta Massoi alizungumza na Jane kwa njia ya simu kutoka Dar es salaam, Tanzania na kuanza kwa kumuuliza manufaa ya radio!

Sauti
5'10"

Wanaume hawana hofu tena kuoa wasichana wasiokeketwa- UNFPA

Ali Haji Hamad, Afisa Jinsia wa UNFPA Tanzania anaangazia; 

Hali ya ukeketaji nchini Tanzania hivi sasa iko vipi?

Nini hasa kichocheo cha mafanikio hayo? 

Maghariba imekuwa ni vigumu sana kuachia zana zao kwa kuwa ni mbinu ya kujipatia kipato. Nini kimefanyika? 

Bila kukeketwa wasichana wanaona aibu kuolewa na wavulana wanaona aibu kuoa mwanamke hajakeketwa. Nini kimefanyika kubadili mtazamo?

Sauti
6'15"
UN News Kiswahili

Penye nia pana njia- Mikoko Pamoja

Wakazi wa Gazi na Makongeni huko Kwale mjini Mombasa nchini Kenya waliamua kushikamana na kulivalia njuga suala la uhifadhi wa mazingira kwa kuanzisha mradi ambao pia unawakwamua katika umasikini.

Mradi huo ujulikanao kama "Mikoko Pamoja" ni wa kwanza kuendeshwa na jamii barani Afrika na umejikita katika upandaji wa mikoko ambayo inatoa hewa ya ukaa.

Sauti
4'11"
UN News/Patrick Newman

UN-Tanzania imefanya mengi kutuelimisha kuhusu SDGs- Rahma

Wiki hii katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani limefanyika kongamano la kimataifa la vijana la mwaka 2018, lenye lengo la kuwajumuisha vijana katika malengo ya maendeleo endelevu au SDGs.

Tulipata fursa ya  kukutana na mmoja wa washiriki wa jukwaa hilo Rahma Abdallah Mwita ambaye ni kijana kutoka Tanzania. Rahma ni mmoja wa wanzilishi wa mtandao  wa vijana kuhusu mabadiliko ya tabianchi ( Youth Climate Change Activist Network).

Sauti
5'22"

Vijana ni ufunguo wa SDGs- Masalu

Vijana wana mchango mkubwa katika kusongesha ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu au SDGs . Hayo yamesisitizwa katika jukwaa la vijana la Umoja wa Mataifa 2018 lililokunja jamvi hii leo kwenye makao makuu ya Umoja huo New York Marekani. Vijana 700 kutoka nchi mbalimbali wamejadili jinsi gani washirikishwe na mchango wao katika kufanikisha azma hiyo ya Dunia. Miongoni mwa waliohudhuria ni kijana Paschal Masalu kutoka nchini Tanzania ambaye ni afisa mtendaji wa jukwaa la Elimikawikiendi nchini humo.

Sauti
3'43"

Kazi ni kazi bora mkono uende kinywani

Vijana hutumia mbinu mbalimbali ili kukidhi  mahitaji ya maisha yao ya kila siku na fani ya ulimbwende au uanamitindo imekuwa ni moja  ya  fani zinazowavutia vijana , kwanza ikiwajengea umaarufu mkubwa lakini pia kuwasaidia kuwa na ajira ya kikidhi mahitaji yao. Hakimu Nkengurutse kijana wa miaka 21 kutoka vijijini  nchini  Burundi amevuka mito na bahari na kutua  nchini Afrika ya Kusini ambako anakofanya kazi ya uanamitindo.

Njombe wafurahia usaidizi wa UN

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo, UNDP Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na wadau wengine wa maendeleo kutoka Uingereza, Marekani na Sweden  na serikali ya Tanzania linajitahidid kutekeleza mpango wa kunusuru kaya masikini (PSSN) kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), ambao kwa sasa umefikia takriban kaya milioni 1.1 wenye umasikini uliokithiri nchini humo...

Sauti
3'31"