Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Baada ya kilio ni faraja kwa familia iliyokimbilia Ubelgiji

Wahamiaji ambao wanajaribu kuvuka bahari ya mediteranea wanakabiliwa na hatari kubwa katika safari zao. Mmoja wa wahanga wa hatari ni mtoto Dina ambapo akiwa na umri wa miezi minne tu akiwa katika nyumba ya msafirishaji haramu nchini Libya aliungua na kupata majeraha kwa asilimia 80 ya mwili wake. Baada ya zaidi ya mwaka mmoja wazazi wake wanatafakari ajali hiyo ambayo huenda ingawalipokonya uhai wa  mtoto wao.Basi ungana na ….. katika makala hii ya wahamiaji walioko Ubelgiji.

Dhibiti tumbaku uongeze kipato- Dkt. Ouma

Hii leo shirika la afya ulimwenguni, WHO limechapisha ripoti yenye kurasa zaidi ya 700 inayoweka bayana faida za kiuchumi za kudhibiti matumizi ya tumbaku na bidhaa zake. Ripoti hiyo inayotokana na utafiti uliofanywa kwa kina inaeleza kuwa hatua mbali mbali zinaweza kuchukuliwa kuhakikisha kuna sera thabiti ambazo kwazo tumbaku inadhibitiwa na hivyo hatimaye serikali inapata kipato, wananchi halikadhalika.

Gueterres kuongoza UM ni sawa na upele kupata mkunaji-Mkimbizi afunguka

Watema Emmanuel, ni mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC. Kwa sasa anaishi nchini Marekani, akiwa ametokea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko Kigoma Tanzania.

Safari yake kuja huku ni sehemu ya mpango wa shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR wa kuwapeleka wakimbizi katika nchi ya tatu na kuwasakia hifadhi na ustawi. Kambini Tanzania, miongoni mwa mambo asiyoyasahau ni kumshuhudia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ambaye wakati huo alikuwa Kamishna Mkuu wa UNHCR. Alifanya ziara nchini humo, na kukutana na wakimbizi.

Harakati za kuimarisha Kiswahili zashika kasi Uganda

Nchini Uganda harakati zinaendelea ili kufanikisha azma ya serikali ya kupanua matumizi ya lugha ya Kiswahili. Harakati hizo ni pamoja na shule za msingi kuchukua hatua kuwapatia wanafunzi stadi mbali mbali za kufanikisha mpango huo wakati huu ambapo Kiswahili ni moja ya lugha rasmi za Muungano wa Afrika, AU. Je nini kinafanyika? Ungana na John Kibego kwenye makala hii kutoka Hoima, Uganda.

Kutana na Erick David Nampesya, mwanahabari gwiji aliyekutana ana kwa ana na Guterres

Akiwa na siku nne pekee ofisini tangu aanze majukumu yake , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, ambaye aliapishwa mnamo Disemba 12 mwaka jana, anaelezwa na wengi kuwa mwenye mwelekeo sahihi wa kukivusha chombo anachokiongoza hususani katika utatuzi wa changamoto za kibinadamu.

Miongoni mwa watu wanaomfahamu ni Erick David Nampesya, mwanahabari mkongwe kutoka Tanzania ambaye alikutana na kumhoji kiongozi huyo miaka kumi iliyopita na anakumbuka vyema mazungumzo yao. Mwanahabari huyo anamweleza Joseph Msami wa idhaa hii kile kilichojiri.

Dola tano tu kwa mwaka yaweza kutibu kifafa: WHO

Ugonjwa wa kifafa unaweza kutibiwa kwa gharama ya dola 5 tu kwa mwaka kwa matumizi ya dawa limesema shirika la afya ulimwenguni WHO.

Kwa mujibu wa WHO, karibu asilimia 70% ya watu wanaotumia dawa hizo kwa muda wa miaka miwili wanaweza kumaliza kifafa.Shrika hilo kupitia mradi wake katika nchi kadhaa limesaidia upatikanaji wa dawa hususani kwa nchi zenye kipato cha kati na zile zinaozendelea

Ungana na Rosemary Musumba katika makala itakayokukutanisha na wahanga wa ugonjwa huo wenye uhusiano na mishipa ya ufahamau.

Fursa adimu kuiwakilisha nchi yangu UM nitaikumbuka daima-Manongi

Balozi tuvako Manongi mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa ambaye sasa anaondoka baada ya kustaafu, amesema kupewa jukumu la kuiwakilisha nchi yako kwenye Umoja wa Mataifa ni jambo la kulienzi na kujivunia kwani ni adimu. Akuzungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii Balozi Manongi pia amempongeza Katibu Mkuu anayeondoka Ban Ki-moon kwa juhudi zake katika mabadiliko ya tabia nchi na malengo ya maendeleo endelevu SDG’s ungana nao katika mahojiano haya.

(MAHOJIANO NA BALOZI MANONGI)

Fidel Castro alikuwa msemaji wa dunia ya tatu:Dr Salim

Fidel Castro alikuwa kiongozi shupavu, jasiri, mtetezi wa wanyonge na kikubwa zaidi alikuwa msemaji wa dunia ya datu hususani nchi za Afrika kutokana na uwazi na kutomuogopa yeyote. Hayo yamejitokeza katika mahojiano maalumu kuhusu mchango wa kiongozi huyo kwa Afrika na kwenye Umoja wa Mataifa, baina ya Flora Nducha na Dr Salim Ahmed Salim.

(MAHOJIANO NA DR SALIM AHMED SALIM)

Wahamiaji Afrika wasaka hifadhi Afrika

Wahamiaji kutoka Afrika kwenda Afrika! Hivi ndivyo unavyoweza kusema kuhusu  maelfu ya wasaka hifadhi na wakimbizi walioko nchini Misri ambao wanasaidiwa na shrike la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi  UNHCR.

Kamishna Mkuu wa UNHCR amewatembelea wasaka hifadhi hao na kuzungumza nao  ili kuwasaidia.

Ungana na Amina Hassan katika makala ifuatayo.