Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Kazi ya ulinzi wa amani UM ni zaidi ya kubeba mtutu wa bunduki

Kikosi kazi cha nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanaochangia vikosi vya kulinda amani kimekuwa kikikutana hapa makao makuu tangu Januari 16 na mkutano wao umehitimishwa leo Ijumaa.

Kikosi hicho kimekuwa kikijadili masuala mbalimbali yanayohusiana na uchangiaji wa vikosi, vifaa, afya na jinsi ya kuboresha huduma kwa nchi wanachama.

Ili kupata undani wa kilichojiri mkutanoni Flora Nducha ameketi na Meja jenerali mstaafu Paul Meela na Meja Jenerali Issa Narsorro walioiwakilisha Tanzania kwenye kikao hicho. Kwanza Meja jenerali Meela anaelezea kuhusu mada zilizotamalaki.

Tatizo la utipwa tipwa

Utipwa tipwa! Nini kinachosababisha hali hii ambayo ni unene wa kupindukia? Kuna wanaosema unene ni urithi wa kuzaliwa nao na kunao wanaoaamini maisha na mazingira vinachangia.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani WHO zaidi ya watu nusu bilioni wana tatizo la utipwa tipwa au unene wa kupita kiasi kote duniani. Hali hiyo inaweza kuleta athari nyingine kama maradhi ya saratani, moyo, kiharusi na ugonjwa wa kisukari. Na njia mojawapo ya kukabili utipwatipwa ni kupunguza vyakula vyeneye mafuta mengi, sukari na chumvi.

Usawa wa kijinsia waleta manufaa nchini Tonga

Ushirikishwaji wa wanawake katika kufanya maamuzi ya kijamii umewezesha maendeleo na utekelezaji wa miradi ya miundombinu mikubwa, kama vile ghati mpya na barabara ya lami katika eneo la Hunga nchi Tonga bahari ya pasifiki, vitu ambavyo kwa miaka mingi hawakuwanavyo. Miradi hii ilizunduliwa na serikali ya Tonga ikishirikiana na shirika la mfuko wa maendeleo ya kilimo, IFAD. Ungana na Selina Jerobon kwa undani zaidi..

Mchango muhimu wa wanawake katika suluhu mzozo wa Colombia ni dhahiri

Yaelezwa kuwa iwapo wanawake watajumuishwa katika mchakato wa amani kuna uwezekano wa asilimia 35 zaidi ya kupatikana makubaliano ambayo yanadumu Zaidi ya miaka kumi na mitano.

Katika Makala hii tunakutana ana kwa ana na mwanamke mmoja wa jamii asili nchini Colombia na mchango wake nchini humo kuanzia athari za mgogoro, mazungumzo na mustakhbali wa hususan wanawake kufuatia mkataba wa amani kutiwa saini. Ungana na Grace Kaneiya

AMISOM watoa mafunzo ya kuukabili ukatili wa kingono na kijinsia Somalia.

Ripoti kadhaa za haki za binadamu barani Afrika, zinaitaja Somalia kama moja ya nchi ambazo ukatili wa kijinsia na kingono hutendeka kwa wingi na kutaka hatua zichukuliwe.

Katika kuhakikisha hilo, ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini humo AMISOM, unatoa mafunzo kwa maafisa wa polisi na jamii juu ya namna ya kukabiliana na ukatili huo. Assumpta Massoi anakupasha kwa undani katika makala ifuatayo.

IFAD/Video Capture

Nishati ya jua yawezesha ukulima wa umwagiliaji - Wanawake Senegal

Shirika la mazingira duniani likishirikiana na mfuko wa maendeleo ya kilimo, IFAD, limezindua mradi wa kuboresha kilimo cha umwagiliaji, ambayo umetekelezwa katika takriban robo ya nchi mzima ya Senegal.

Katika makala hii, tunakutana na kikundi cha wanawake kiitwayo "Takku ligguaey de Taiba" ambacho ni moja ya vikundi ambavyo wamepata kunufaika na Mradi huu. Ungana na Amina Hassan..

Machozi na furaha watoto wakikutanishwa na wazazi wao nchini Sudan Kusini

Kulingana na takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, takriban watoto 4,000 wamekutanishwa na wazazi wao tangu vita na vurugu uzuke nchini Sudan Kusini mwaka 2013. Kambi la wakimbizi wa ndani, Bor, lilitengwa kwa ajili ya watoto waliotenganishwa na wazazi wao, lengo kubwa likiwa ni kuwawezesha watoto hao kuenda shule.

Katika makala hii, tunakutana na mtoto wa kike Nyanaeda ambaye ni mmoja wa watoto wakimbizi nchini humo waliokutanishwa na wazazi. Ungana na Flora Nducha kwa undani zaidi...

Tatizo la msongo wa mawazo na athari za afya ya akili

Kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni WHO, msongo wa mawazo ambao ni mvurugano katika akili hutokana sababu kadhaa kama vile mkwamo katika uhusiano, uchumi na mengineyo, huwakumba mtu mmoja kati ya wanne kwa nyakati tofauti.

Kwa takribani watu milioni 350 duniani wameathiriwa na msongo wa mawazo. WHO inasema, unyanyapaa dhidi ya wagonjwa, huzuia watu wengi kutafuta msaada.

Kama hiyo haitoshi, zaidi ya asilimia 75 ya watu wanaokabiliwa na ugonjwa huu katika nchi zinazoendelea  hawapati matibabu.

Rumba ya Cuba ni turathi iliyotuzwa na UNESCO

Rumba ya Cuba inahusishwa na utamaduni wa Afrika lakini pia inachanganya na utamaduni wa hispania. Utamaduni  huu nchini Cuba umeshamiri zaidi kwenye vitongoji vya watu wa kipato cha chini na vijijini kuanzia magharibi hadi mashariki mwa nchi hiyo. Miondoko yake, mbwembwe na hisia zitokanazo na mtindo huu wa dansi ni dhihirisho la utamaduni ambao shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO limetambua na kuingiza kwenye orodha ya turathi za tamaduni zisizogusika za kibinadamu. Je rumba hii nini hasa?

Simulizi ya mtoto Ahmed aliyenusurika vitani Iraq

Baada ya mazonge ya vita, manusura huathirika kwa namna kadhaa ikiwamo kiuchumi, kijamii na hata kisaikolojia. Hili liko dhahiri nchini Iraq ambapo mapigano kati ya vikosi vya serikali na kundi la kigaidi la ISIL yanaendelea.

Katika makala ifuatayo Rosemary Musumba anamulika juhudi za kuwasaidia vijana baada ya athari za kivita nchini humo ambapo Umoja wa Mataifa kushirikiana na wadau unatoa usaidizi wa kijami na kisaikolojia, ungana naye.