Umuhimu wa vyoo na huduma za kujisafi
Nyumba ni choo! Huu ni usemi ambao hutumika mara nyingi ukiangazia umuhimu wa choo bora na huduma za kujisafi nyumbani.
Tarehe 19 mwezi huu ilikuwa ni siku ya choo duniani. Dunia imekumbushwa kuwa choo na huduma za kujisafi ambazo hazipewi umuhimu zaweza kuchangia ukuaji wa uchumi.
Umoja wa Mataifa katika taarifa yake umesema maadhimisho ya mwaka huu yana maudhui ya vyoo na ajira na umuhimu wa huduma za kujisafi au ukosefu wake katika ustawi na mazingira ya kazi.