Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Gueterres kuongoza UM ni sawa na upele kupata mkunaji-Mkimbizi afunguka

Gueterres kuongoza UM ni sawa na upele kupata mkunaji-Mkimbizi afunguka

Pakua

Watema Emmanuel, ni mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC. Kwa sasa anaishi nchini Marekani, akiwa ametokea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko Kigoma Tanzania.

Safari yake kuja huku ni sehemu ya mpango wa shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR wa kuwapeleka wakimbizi katika nchi ya tatu na kuwasakia hifadhi na ustawi. Kambini Tanzania, miongoni mwa mambo asiyoyasahau ni kumshuhudia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ambaye wakati huo alikuwa Kamishna Mkuu wa UNHCR. Alifanya ziara nchini humo, na kukutana na wakimbizi.

Katika mahojiano na Joseph Msami wa idhaa hii, Emmanuel anasimulia kitu kilichomsahangaza wakati wa ziara hiyo anachokiunganisha na uteuzi wa Guterres kuwa Katibu Mkuu wa UM akisema ni mtu sahihi kwa changamoto za sasa.

Photo Credit
Watema Emmanuel.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/Binafsi)