Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Radio ni tegemeo katika kuendesha shughuli za kipato Tanga, Tanzania

Radio ambayo ni chombo cha mawasiliano inatajwa kuwa muhimu katika kutoa taarifa iwe ni habari kuhusu matukio mbali mbali ulimwenguni au taarifa kuhusu bei ya vyakula sokoni au hali ya hewa. Taarifa kama hizi ni muhimu kwa jamii husika kwani zinatumika katika kuendesha kazi za kila siku, mathalani kilimo au uvuvi.

Umuhimu wa radio katika nyanja hizo umedhihirika katika makala hii ya Martha James wa radio washirika Pangani FM kutoka Tanga nchini Tanzania.

Redio, muziki na vijana!

Muziki na ujumbe! Ndivyo unavyoweza kusema ukiangazia namna muziki unavyotumiwa na vijana katika redio ili kuelimisha umma, juu ya masuala kadhaa ikiwamo afya, ajira na hata ushiriki wa kundi hilo katika siasa.

Kuelekea siku ya redio duniani Februari 13, Rosemary Musumba ameangazia redio katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara na umuhimu wa muziki katika vipindi vya redio hizo za vijana. Ungana naye.

Miaka 10 sasa bila mtoto wa kike au mwanamke kukeketewa Olepolos Kenya

Umoja wa Mataifa ukipigia debe hatua za kutokomeza ukeketaji dhidi ya watoto wa kike na wanawake kote ulimwenguni, nchini Kenya harakati zinazidi kushika kasi na hata kuna nuru kwani wakazi wa Olepolos katika nchi hiyo wa Afrika Mashariki hawajashika kiwembe kumkeketa mtoto wa kike au mwanamke kwa miaka kumi sasa. Je nini wamefanya nini? Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza kwa njia ya simu na Caroline Murgor, mratibu wa kitaifa wa mradi wa pamoja wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, na lile la idadi ya watu, UNFPA wa kutokomeza FGM nchini Kenya.

WHO yazindua mwongozo wa kukabili saratani

Leo ni siku ya saratani duniani ambapo shirika la afya duniani, WHO linazindua mwongozo mpya wa kuwezesha uchunguzi wa mapema wa ugonjwa huo hatari unaosababisha vifo vya watu milioni 8.8 kila mwaka duniani, kati ya wagonjwa milioni 14 wanaobainikana ugonjwa huo.

WHO inasema hali si shwari kwani idadi inaongezeka mwaka hadi mwaka na hivyo njia pekee ni kuimarisha mbinu za kubaini mapema kwani hata visababishi vya saratani navyo vinaongezeka.

Utamaduni wa Oromo uliotambuliwa na UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO linaendeleana kazi yake ya kubaini tamaduni za aina yake ulimwenguni ambazo zinapaswa kuhifadhiwa ili ziweze kuendelea kurithiwa kizazi na kizazi. Mojawapo ni mfumo wa kisiasa, kiuchumi na kijamii wa kabila la Oromo nchini Ethiopia. Mfumo huo wa maisha unarithishwa kwa njia ya simulizi na tayari UNESCO umeingiza katika orodha ya turathi za tamaduni zisizogusika za kibinadamu. Je ni aina gani? Assumpta Massoi anasimulia kwenye makala  hii.

UNMISS yatembelea Kajo Keji kujionea hali halisi

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS unasema kuwa karibu wakimbizi wa ndani 1800 kwenye eneo la Kajo Keji nchini wanahitaji msaada wa dharura. Japokuwa wakimbizi hawa wamejipata kwenye kambi za wazi kwa muda mrefu lakini kuna nuru ya matumaini walipotembelewa na maafisa wa UNMISS na wale wa kutoka kwa shirika la kiserikali linalohusika na masuala ya maendeleo pembe ya Afrika, IGAD. Ungana na Flora Nducha akiangazia yanayoendelea kwenye eneo hilo....

WFP yaleta nuru kwa wenyeji kambi ya Nyarugusu, Tanzania

Nchini Tanzania, shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limeanza kuwapatia wakimbizi  10,000 fedha taslimu ili kujinunulia chakula badala ya kutegemea chakula chote kupitia mgao. Mradi huo ni wa majaribio na umeanza mwezi uliopita wa Disemba ambapo WFP inasema imewezekana baada ya kupata mchango wa dola za kimarekani 385,000 kutoka Canada. Je nini kinafanyika?

Tanzania ichukue hatua kwenye matumizi ya mkaa

Hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, Erick Solheim alikuwa ziarani nchini Tanzania kujionea harakati za nchi hizo za uhifadhi wa mazingira na changamoto ambazo inakumbana nazo. Miongoni mwa watu aliokutana nao ni wachuuzi wa mkaa ambapo yaelezwa kuwa biashara hiyo huingizia Tanzania dola bilioni Moja kwa mwaka.