Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Biashara haramu ya tumbaku yaanza kubanwa

Hatimaye itifaki ya kutokomeza biashara haramu ya bidhaa za Tumbaku imeanza kutiwa saini na hivyo kuonyesha utashi wa kisiasa wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa kudhibiti matumizi ya tumbaku. Hafla hiyo ilifanyika mjini Geneva Uswisi kwa mataifa 12 wanachama wa mkataba huo kutia saini na baadaye shughuli hiyo itahamishiwa New York, Marekani makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa nchi nyingine wanachama wa Mkataba huo kuweza kutia saini. Assumpta Massoi amefuatilia hafla hiyo na hii ni ripoti yake.

(SAUTI YA ASSUMPTA MASSOI)

Kurejea kwa wakimbizi wa Somalia ni vema lakini kuna changamoto

Mwezi huu wa januari kumeshuhudiwa kuanza kurejea kwa wakimbizi wa Somalia nchini mwao.

Tafsiri mbalimbali zimetolewa juu ya kitendo hicho lakini kubwa zaidi likielezwa kuwa ni kurejea kwa amani nchini Somalia baada ya miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hata hivyo ili kufahamu zaidi Monica Morara wa radio ya Umoja wa Mataifa amefanya mahojiano maalum na mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Balozi Augustine Mahiga ambaye anaanza kwa kuelezea hatua hiyo ya kurejea nyumbani kwa wakimbizi

(MAHOJIANO BALOZI MAHIGA)

IFAD yakomboa wanawake Gambia

Kilimo bora kinahitaji pia uwepo wa ardhi yenye rutuba. Nchi Gambia kama ilivyo katika nchi nyingi za Afrika tunaelezwa kuwa ardhi yenye rutuba hutumiwa zaidi na wanaume na wanawake hubakia pembezoni kwenye ardhi iliyochoka na hivyo hata kwa jitihada gani matunda ya kazi ni nadra kuonekana. Lakini kwa sasa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD umeleta matumaini kwa wanawake hao. Je nini kimefanyika? Ungana na Assumpta Massoi katika ripoti hii.

Mradi wa maji waleta nuru kambi ya Dadaab

Kambi ya Dadaab iliyoko Kaskazini Mashariki mwa Kenya inahifadhi wakimbizi kutoka Somalia. Kambi hii inaelezwa kuwa ni kubwa kuliko kambi zote za wakimbizi duniani ikiwa inahifadhi wakimbizi zaidi ya Laki Nne na Nusu. Uhaba wa maji umekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo. Lakini nuru imechomoza na kubadili maisha ya familia za kifugaji. Ni nuru gani hiyo? Ungana na Assumpta Massoi kwa ripoti kamili:

Soundbite 1: Play then hold under

Azimio la UM kwa UNEP ni la kihistoria na linatoa fursa zaidi kwa wanachama wa UM: Steiner

Mwezi Disemba mwaka 2012 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio kuhusuu shirika lake linalohusika na mazingira, UNEP. Je azimio hilo lina malengo yapi na manufaa yake ni nini? Tujiunge na Monica Morara.

"We now take a decision on draft resolution entitled, Report of the Governing Council of the United Nations Environment Programme …. The Second Committee adopted the resolution without a vote. May I take it that the assembly wishes to do likewise? It is so decided."

Kampuni ya sukari ya Mumias nchini Kenya na uhifadhi wa mazingira

Harakati za viwanda kujaribu kuhifadhi mazingira kwa kutumia mabaki ya malighafi za bidhaa zake kuzalisha bidhaa nyingine zinazidi kushika kasi, na viwanda kuwa mifano kwa viwanda vingine kama njia mojawapo ya kuhifadhi mazingira huku zikijiibulia huduma zingine. Miongoni mwa viwanda hivyo ni kile cha sukari cha Mumias nchini Kenya ambacho sasa kinazalisha umeme kwa kutumia rojo zito la sukari, ambayo ni mabaki yatokanayo na uzalishaji wa bidhaa yake, Sukari. Assumpta Massoi na ripoti kamili:

(SAUTI YA ASSUMPTA MASSOI)

Vita dhidi ya Malaria yakwamishwa na pesa: Tanzania Zanzibar, Rwanda na Zambia zang’ara katika kutokomeza Malaria

Ripoti mpya ya shirika la afya duniani, WHO kuhusu ugonjwa wa Malaria kwa mwaka 2012 imeonyesha kupungua kwa ufadhili katika mipango ya vita dhidi ya ugonjwa huo uliosababisha vifo vya watu takribani Laki Sita na Elfu Sitini duniani kote.

Idadi kubwa ya vifo hivyo ni vya watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano. Hata hivyo ripoti hiyo inaonyesha mafanikio katika baadhi ya nchi mathalani Tanzania upande wa Zanzibar ambapo maambukizi kwa sasa ni asilimia Sifuri.

Hofu ya usalama, mila na desturi zakwamisha matumizi ya vyoo

Umaskini pamoja na mila na desturi ni baadhi ya mambo yanayosababisha usafi duni miongoni mwa nchi maskini. Usafi huu duni unamulika zaidi matumizi ya vyoo salama ambapo inaelezwa kuwa kutokana na baadhi ya mila baadhi ya watu wanalazimika kujisaidia haja kubwa vichakani na hivyo kuhatarisha kuenea kwa magojwa kama vile kipindupindu.