Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Azimio la UM kwa UNEP ni la kihistoria na linatoa fursa zaidi kwa wanachama wa UM: Steiner

Azimio la UM kwa UNEP ni la kihistoria na linatoa fursa zaidi kwa wanachama wa UM: Steiner

Pakua

Mwezi Disemba mwaka 2012 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio kuhusuu shirika lake linalohusika na mazingira, UNEP. Je azimio hilo lina malengo yapi na manufaa yake ni nini? Tujiunge na Monica Morara.

"We now take a decision on draft resolution entitled, Report of the Governing Council of the United Nations Environment Programme …. The Second Committee adopted the resolution without a vote. May I take it that the assembly wishes to do likewise? It is so decided."

Mwakilishi wa kudumu wa Lebanon katika Umoja wa Mataifa, Nawaf Salam akiwasilisha rasimu ya azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu shirika la kimataifa la Mazingira, UNEP.  Hiyo ilikuwa ni tarehe 21 mwezi Disemba, ambapo Umoja wa Mataifa ulipitisha azimio hilo la kuongeza hadhi ya UNEP kwa kuweka wazi fursa kwa nchi zote wanachaam 193 ndani ya bodi ya uongozi wa shirika hilo. Azimio la kuongeza fursa hizo kutoka 58 hadi nchi zote 193 ni kiashiria kuwa Umoja wa Mataifa unaimarisha uwezo wa UNEP katika harakati zake za uhifadhi wa mazingira duniani kwa kuweka ajenda ya dunia ya kulinda mazingira.

Halikadhalika uamuzi huo ni utekelezaji wa baadhi ya matakwa ya nyaraka kuu iliyotokana na mkutano wa Rio + 20 uliofanyika Brazili mwaka huu. Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP Achim Steiner akazungumzia uamuzi huo izungumzia uamuzi huo amesema

(SAUTI YA STEINER)

Kwa mara ya kwanza, ndani ya miaka 40, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimeandika upya katiba ya UNEP kwa kutoa fursa ya uanachama kwa mataifa yote wanachama wa Umoja wa Mataifa na hivyo kulipa shirika hilo mtazamo mpya juu ya dhima yake, mtazamo wake na umuhimu wake ndani ya familia ya Umoja wa Mataifa.”

Bwana Steiner amesema kwa fursa sawa za ushiriki miongoni mwa wanachama, UNEP itakuwa kitovu cha udhibti wa mazingira na maendeleo endelevu na kwamba uamuzi huo ni wa kihistoria.

(SAUTI YA STEINER)

Kwa UNEP na jamii ya kimataifa ya kulinda mazingira na kwa maendeleo endelevu, hii naamini ni wakati wa kihistoria.”

Taarifa ya UNEP inasema kuwa azimio hilo linawezesha shirika hilo kupata fedha kutoka bajeti ya kawaida ya Umoja wa Mataifa na kutaka wahisani wa shirika hilo kuongeza ufadhili wao wa kujitolea. Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilianzisha UNEP baada ya mkutano wa mwaka 1972 huko Stockholm Sweden kuhusu mazingira ya binadamu kwa lengo la kufanya mazingira kuwa ajenda ya kimataifa na kulitaka shirika hilo kusaidia nchi wanachama kuratibu sera za mazingira.

Naam asante sana Monica Morara kwa ripoti hiyo kuhusu azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lililobadili hadhi ya UNEP ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miongo minne.