Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Sehemu za ibada zatumika kutoa tiba Uganda: UNICEF

Huduma ya afya ya msingi ni jambo muhimu kwa jamii ili waweze kushiriki shughuli za maendeleo. Hata hivyo katika maeneo mengi ya nchi zinazoendelea Uganda ikiwa ni mojawapo, watu hulazimika kwenda mwendo mrefu kupata huduma hizo na hivyo kusababisha kukosa huduma au kuipata wakati wameshachelewa. Kwa mantiki hiyo Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, limebuka na mpango mpya nchini Uganda. Je ni upi huo? Ungana na Joseph Msami katika ripoti hii.

MONUSCO yapambana na waasi DRC Kongo,juhudi zaidi zahitajika

Kongo DRC ni nchi ya pili kwa ukubwa barani Afrika yenye rasilimali nyingi, ikiwemo madini na uoto wa asili. Nchi hii yenye idadi ya zaidi ya watu milioni sabini ina historia ndefu ya mapigano yaliyosababisha maafa kadhaa ikiwamo vifo, ulemavu na hata wakimbizi wa ndani ya nchi na wale waliokimbilia nchi jirani kutafuta hifadhi.

Mwishoni mwa mwezi February umeripotiwa mapigano katika kijiji cha Kitchanga kati ya kundi la Wanamgambo linalofahamika kama Muungano wa Wazalendo kwa ajili ya Kongo iliyo huru na inayojitegemea (APCL) na jeshi la serikali ya Kongo DRC (FARDC).

Ushirikiano wahitajika kudhibiti wizi wa haki miliki: WIPO

Suala la haki miliki linaelezwa kuwa bado linaendelea kuzua utata na kukwamisha matumizi stahili ambayo yanaweza kusaidia nchi kujikwamua kiuchumi.

Barani Afrika ripoti zinaonyesha kuwa mapato mengi hupotea kutokana na kukithiri kwa vitendo vya wizi wa haki miliki, kunafanyika kwenye maeneo mbalimbali.

Ni kwa mantiki hiyo wataalamu wanakutana jijini Dar es Salaam katika mkutano ulioandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la hakimiliki, WIPO na serikali ya Tanzania. George Njogopa ametuma taarifa hii.

UNMISS yatoa mafunzo ya lugha ya kiingereza kwa polisi wa kike

Dunia ikiwa imeadhimisha siku ya wanawake Machi Nane ambapo tumeshuhudia maadhimisho hayo yakifanyika kwa matukio mbalimbali ikiwemo matembezi na kadhalika, nchini Sudan Kusini,Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS, umetumia maadhimisho ya siku ya wanawake kwa kufundisha  Kiingereza  wanawake zaidi ya 50.  Mafunzo hayo yanafanyika katika hema lililoko katika karakana iliyoko katika kituo cha polisi Sudan Kusini ambapo askari wanawake wanaofundishwa lugha ya Kiingereza iliyo miongoni mwa lugha rasmi ya nchi  ni kutoka Jeshi la Polisi la nchi hiyo.Ungana na Joseph

Tafiti zaidi zahitajika kubaini kiwango cha ukatili wa kijinsia: TAMWA

Siku ya wanawake duniani ni fursa ya kutathmini hatua zilizochukuliwa kulinda hadhi na ustawi wa mwanamke na mtoto wa kike. Nchini Tanzania, chama cha waandishi wa habari wanawake, TAMWA kiliendesha utafiti kubaini kiwango cha ukatili wa kijinsia, utafiti uliofanyika katika wilaya Kumi nchini humo. Je nini kilibainika? Na matokeo ya utafiti huo yanalenga kuboresha nini? Basi ungana na Stella Vuzo wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa mjini Dar es salaam Tanzania katika mahoajiano yake na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Valeri Msoka. Valerie anaanza kwa kutaja wilaya husika.

UNMISS yatoa elimu juu ya kazi na wajibu wa ujumbe huo Sudan Kusini

Katika kutoa elimu juu ya wajibu na majukumu ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini (UNMISS) katika jamii ya jimbo la Jonglei, ujumbe huo ulizuru jamii ya watu wa AKUIDENG BOMA, mji ulioko Jalle Payam takribani kilometer 60 kutoka mji unaofahamika kama Bor.

Ungana na Joseph Msami katika makala hii inayomulika juhudi za UNMISS katika kuwaelimisha raia namna ya kushirikiana na ujumbe huo kukomesha mapigano na kuleta amani ambayo imekuwa ni adimu nchini Sudan Kusini, taifa lililozaliwa mwezi Julai mwaka 2011.

UNICEF na washirika wasaidia waathirika wa Kipindupindu Haiti

Haiti nchi iliyoko katika visiwa vya Karibia ni nchi ambayo imekumbwa na ugonjwa wa mlipuko wa kipindupindu .Hii inatokana na majanga mbalimbali ya kibinadamu kama vile matetemeko ya ardhi yaliyosababisha watu wengi kukosa makazi na hivyo kuishi katika mazingira hatarishi.

Mlipuko wa kipindupindu umechangiwa na mikusanyiko ya watu katika nyumba zisizo rasmi, yakiwemo mahema, huku pia sababu nyingine inayotajwa kuchangia ugonjwa huo unaodhoofisha na kuua haraka ni misongamano mikubwa ya nyumba na matumizi mabaya ya huduma za kijamii kama vile maji na hata vyakula.

UNICEF yakomboa shule ziliizoteketezwa na kimbunga Madagascar

MADAGASCAR! Kisiwa ndani ya bahari ya HINDI kilichoko Kusini Mashariki mwa Afrika chenye idadi ya watu  zaidi ya milioni 22.

Kisiwa hiki kimekuwa kikikumbwa na vimbunga mara kadhaa! Vimbunga hivi vimekuwa vikiathiri sekta  mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Leo katika makala tunamulika namna ambavyo vimbunga hivi vimeathiri sekta ya kilimo chini Madgascar na mchango wa umoja wa matiafa  katika kuzinusuru shule hizo.

Ungana na Joseph Msami katika makala hii ili ufahamu kulikoni vimbunga Madagascar?