Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

UNICEF na washirika wakomboa watoto kutoka ajira migodini huko DRC

Ajira kwa watoto watoto ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazokabili nchi zinazoendelea. Katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC hali ni mbaya zaidi. Nchini humo sio ajabu kuwaona  watoto wenye umri wa kwenda shule wakifanya kazi za kujipatia kipato ambazo hata hivyo huwaingizia kipato kidogo  ikilinganishwa na kazi wanazofanya. Mwenzangu JOSEPH MSAMI anamulika adha wanazokutana nazo watoto wanapokuwa katika migodi ya uchimbaji almasi huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo DRC, ambayo ndiyo nchi yenye almasi  nyingi zaidi duniani.

Watoto, wazazi wajikita kwenye elimu huko Turkana

Imezoeleka ya kwamba sehemu kubwa ya jamii ya wafugaji imekuwa nyuma kielimu husuani katika elimu ya msingi ambapo watoto wenye umri wa kwenda shule wamekuwa hawafanyi hivyo. Badala yake, watoto hawa hutumia muda mwingi kuchunga mifugo nakufanya kazi nyingine za nyumbani. Huko nchini Kenya katika eneo la Turkana kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo, mambo yalikuwa hivyo  lakini sasa hali ni tofauti. Watoto wengi wenye umri wa kwenda shule katika jamii hii ya kifugaji wanakwenda shule.

Quinoa zao la kumkomboa mkulima, lastahimili ardhi kame!

Hatimaye mwaka wa kimataifa wa zao la Quinoa umezinduliwa rasmi kwenye kikao maalum cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani. Shughuli hiyo imeshudiwa na viongozi na wawakilishi wa mataifa na mashirika mbali mbali akiwemo Rais wa Bolivia, Evo Morales ambaye nchi yake ndiyo inaongoza duniani kwa kuuza zao hilo nje ya nchi. Tayari tumeelezwa kuwa zao la Quinoa, ambayo ni nafaka itokanayo na mbegu za mmea huo jamii ya spinachi, limeenea nchi mbali mbali duniani ikiwemo Kenya na kutoa matumaini ya kutokomeza njaa na umaskini miongoni mwa wakulima.

Radio kuendelea kuwepo leo, kesho na milele: Mbotela

Katika ukanda wa Afrika Mashariki, jina Leonard Mambo Mbotela ni maarufu sana kutokana na vile ambavyo mtangazaji huyo mkongwe wa Radio wa nchini Kenya alivyoweza kumudu mikrofoni yake na kuwasiliana na msikilizaji kila uchwao. Miongoni mwa vipindi tulivyofanya katika kuadhimisha siku ya radio duniani ni mahojiano na mtangazaji huyo mkongwe kuhusu mambo mbali mbali ikiwemo hatma ya radio katika zama za maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano pamoja na dhima ya radio na uchaguzi wa Kenya.

Wadhaniao huduma za posta zinakufa wanaota ndoto ya mchana: UPU

Kadri maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano yanavyozidi kuibuka, baadhi ya watu wamekuwa na hofu juu ya hatma ya huduma za posta, wakidhani kuwa matumizi ya barua pepe, simu za mkononi na hata utumaji wa pesa kwa mtandao ni hati ya kifo kwa huduma za posta. Mkurugenzi Mkuu wa muungano wa mashirika ya posta duniani, UPU, Bishar Hussein anasema La hasha! Sasa ndio huduma za posta zinashamiri kwani teknolojia ya mawasiliano mathalani imeibua huduma mbali mbali ikiwemo biashara mtandao.

IOM yasaidia wahanga wa mafuriko Zimbabwe

Mvua kubwa zilizoanza kunyesha katikati ya mwezi huu huko Zimbabwe zimesababisha mafuriko ambayo yameharibu miundombinu ya kijamii na kiuchumi ikiwemo barabara na shule.

Maelfu ya watu kwa sasa hawana makazi na wanahitaji msaada ambapo shrika la kimataifa la uhamiaji, IOM, kwa kushirikiana na idara ya ulinzi wa raia nchini Zimbabwe wameitikia wito wa kutoa misaada kwa wahanga wa mafuriko hayo.

Utupaji na upotevu wa chakula sasa basi: UM

Katika harakati za kuona kuna uhakika wa chakula duniani, kampeni mpya imeanzishwa kuepusha upoteaji au utupaji wa chakula. Kampeni hiyo inayoendeshwa na shirika la chakula na Kilimo duniani, FAO na lile la mazingira, UNEP kwa kushirikiana na wadau wao inazingatia kuwa maelfu ya Tani za chakula hupotea na kusababisha hasara ya dola Trilioni Moja. Je kwa nini hali hii wakati kila uchwao ni kilio cha ukosefu wa chakula? Ungana na Alice Kariuki katika ripoti hii.

AU yazungumzia Madagascar na Mali

Umoja wa Afrika umekaribisha hatua ya rais wa Madagascar Andry Rajolina ya kutangaza kutogombea kwenye uchaguzi mkuu wa urais uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu, ikiwa ni sehemu kukubali sharti lililkotoewa na Jumuiya ya Maendeleo Kusin mwa Afrika SADC, iliyotaka kuwepo kwa maelewano ya kisasa ili kuondosha hali ya uhamasama iliyoliandama taifa hilo kwa miaka kadhaa. HAlikadhalika Umoja wa Afrika umezungumzia operaioni za kijeshi zinzoendelea huko mali dhidi ya vikundi vyenye silaha chini Mali.

Kutoka DSM, George Njogopa anaarifu zaidi