Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Mtihani wa kujiunga na UM kwa vijana waliobobea kitaaluma, 2012

Je, wewe ni kijana ambaye amehitimu na shahada ya digrii, na unaongea lugha ya Kiingereza au Kifaransa sanifu? Je, ungependa kufanya kazi na Umoja wa Mataifa? Mtihani wa vijana waliobobea kitaaluma, na ambao wangependa kujiunga na Umoja wa Mataifa kwa mpango wa vijana waliobobea, yaani YPP, utafanyika Disemba 12, 2012.

Kuna nafasi katika idara kadha wa kadha za Umoja wa Mataifa, ikiwemo idara ya habari, ambako watayarishaji wa vipindi wanahitajika katika lugha za Kireno na Kiswahili.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yaitaka serikali ya Tanzania kulifungulia gazeti

Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Tanzania yameikosoa serikali kwa jinsi inavyotendea  uhuru wa vyombo vya habari na wakati huo huo yametoa siku saba kwa serikali hiyo kulifungulia gazeti moja ililolifungia vinginevyo yataanzisha maandamano ya amani nchi nzima.

Mashirika hayo ni yale yanayotetea ustawi wa kijamii yakiwemo kituo cha sheria na haki za binadamu, Mtandao wa jinsia TGNP, na taasisi vya vyombo vya habari kusini mwa afrika MISA.

Kutoka DSM, George Njogopa anaarifu zaidi

Vijana kwenye mstari wa mbele wa kutaka watambuliwe kama watu wenye manufaa kwenye jamii

Huku mamilioni ya vijana wakiwa hawana ajira kote duniani baadhi yao wameamua kwamba ni vyema wajitokeze, wajionyesha na kujitambusha kwenye sekta mbali mbali duniani angalau kutambuliwa kama walio wenye manufaa makubwa kwa jamii. Baada ya kutambua kuwa hawashirikishwi vilivyo kwenye masuala yanayowahusu baadhi yao wamebuni mashirika yanayowaleta pamoja hasa wanafunzi wanaosomea taaluma mbali mbali na kusafiri nchi tofauti kuonyesha uwezo walio nao na vipawa vyao na kutaka wapewa nafasi ya kuvitumia hasa katika kutimizwa kwa malengo ya Milenia.

Baada ya miaka Takribani 40 Somalia yapata Katiba Mpya:Mahiga

Viongozi wa serikali ya mpito ya Somalia na wawakilishi wa majimbo yote ya nchi hiyo wanaokutana Moghadishu wamepitisha kwa wingi wa kura katiba mpya  ambayo inafungua mlango wa kuchaguliwa kwa serikali mpya mwezi huu. Jumla ya wawakilishi 825 walikuwa wakijadili kuhusu katiba hiyo kwa juma zima na 621 wamepiga kura ya ndiyo, 13 wamepinga na 11 hawakupiga kura kabisa.Kwa mujibu wa mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini humo balozi Augstine Mahiga huu ni mwanzo wa ukurasa mpya Somalia, na viongozi wanathibitisha kuheshimu mchakato wa kisiasa nchini humo.

Kituo cha haki za binadamu Tanzania chalaumu kuvunjwa kwa haki za binadamu

Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania leo kimetangaza ripoti yake ya awali inayoangazia mwenendo wa haki za kibinadamu kwa nchi hii katika kipindi cha miezi sita iliyopita na kutaja kasoro kadhaa ikiwemo kushamiri kwa matukio ya ubakaji unawandama hasa wanawake na watoto wa shule pamoja na vyombo vya dola kuangukia kwenye lawama ya utumizi mabaya wa madaraka.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Wataalamu wa uvuvi barani Afrika wakutana Tanzania kujadilia sekta hiyo

Wataalamu kutoka sehemu mbalimbali barani afrika wameanza mkutano wao wa siku nne jijini dar es salaam nchini Tanzania kujadilia kile kinachoitwa uchumi wa uvuvi wa samaki ambao unaripotiwa kukua kwa kasi lakini ukiandamwa changamoto ya kushamiri kwa uvuvi haramu.

Kutoka DSM, George Njogopa ameandaa taarifa ifutayo inayoangazia mkutano huo ambao pia umejuisha wataalamu kutoka nchi za Ulaya.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Vyama vya Siasa Afrika vyakutana Tanzania Kujadilia Ufadhili wa Fedha

Makundi ya kisiasa barani afrika yameanza mkutano wa siku tatu nchini Tanzania kwa shabaha ya kujadilia nafasi ya vyama vya kisiasa pamoja na mwelekeo mpya wa ufadhili wa mafungu ya fedha.

Wajumbe kwenye mkutano huo ambao umefunguliwa na makamu wa rais Dr Gharib Bilal wanatazamia kumulika nafasi ya vyama vya siasa nanma vinavyoweza kushiriki kwenye ujenzi wa demokrasia na wakati huo huo kuwavutia wapiga kura katika mazingira ya amani na utulivu.