Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto, wazazi wajikita kwenye elimu huko Turkana

Watoto, wazazi wajikita kwenye elimu huko Turkana

Pakua

Imezoeleka ya kwamba sehemu kubwa ya jamii ya wafugaji imekuwa nyuma kielimu husuani katika elimu ya msingi ambapo watoto wenye umri wa kwenda shule wamekuwa hawafanyi hivyo. Badala yake, watoto hawa hutumia muda mwingi kuchunga mifugo nakufanya kazi nyingine za nyumbani. Huko nchini Kenya katika eneo la Turkana kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo, mambo yalikuwa hivyo  lakini sasa hali ni tofauti. Watoto wengi wenye umri wa kwenda shule katika jamii hii ya kifugaji wanakwenda shule. Kwa undani zaidi wa taarifa hii ungana na Joseph Msami anayezungumzia elimu katika jamii ya wafugaji wa kimasai.