Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Kuelekea kikomo cha MDGs Burundi yapiga hatua, elimu

Ikiwa kikomo cha malengo ya milenia kinakaribia mwaka 2015 nchi mbalimbali zinajitahidi kufikia malengo hayo ambapo  nchini Burundi nchi iliyoko Afrika Mashariki, imepiga hatua katika kuandikisha elimu ya msingi kwa watoto wanaosatahili.

Mathalani takwimu zinonyesha kwamba mwaka 2004 wavulana na wasichana walioandikishwa kuanza elimu ya msingi nchini Burundi ni asilimia 57.

Kuelekea siku ya afya duniani, mfumo wa maisha wachochea magonjwa

Takiwmu za shirika la afya duniani WHO zinaonyesha kwamba Kila mtu mzima mmoja kati ya watatu duniani ana ongezeko la shinikizo la damu, hali ambayo inasababisha karibu nusu ya vifo vyote vitokanavyo na kiharusi, na maradhi ya moyo.

Takwimu hizi ni kutokana na ripoti mpya ya shirika la afya duniani ambayo pia inasema mtu mzima mmoja kati ya kumi duniani ana ugonjwa wa kisukari.

 AMISOM yatoa mafunzo ya kijeshi Somalia

Vikosi vya muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM vimekuwa vikitoa misaada kadhaa ya kijeshi ikiwemo kusaidia katika ulinzi na usalama wa nchi hiyo ambayo imeshuhudia mizozo kwa miongo kadhaa.

Misaada ya AMISOM imekwenda mbali  ambapo sasa wanatoa mafunzo ya kijeshi kwa majeshi ya nchi hiyo.

Hivi karibuni Umoja wa Ulaya ulitoa msaada wa euro milioni 33 kwa vikosi hivyo ili kusaidia kuimarisha na kujenga upya serikali ya Somalia.

Hali yazidi kuwa tete kwa wahamiaji nchini Yemen, IOM yarejelea ombi la msaada

NchiniYemen, shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM linaendelea kutoa ombi la kupata dola Milioni Tano kwa ajili ya kusaidia wakimbizi waEthiopianaSomaliawaliokwama nchini humo baada ya kushindwa kuendelea na safari zao za ughaibuni. Mazingira ya kibinadamu ni magumu, wengine wanafariki dunia na wengine hususan wanawake na watoto wako hatarini kukumbwa na ukatili. Uhasama umeshamiri baina ya wenyeji na wahamiaji. Jumbe Omari Jumbe, msemaji wa IOM aliulizwa na Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali halisi ya kibinadamu na hatma ya usaidizi.

Wahamiaji wa Kiethiopia na Kisomali wakwama Yemen IOM yaomba msaada

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM nchini Djibouti  limetoa ombi la dharura la dola Milioni Tano kwa ajili ya kuokoa maisha ya wahamiaji wa Ethiopia na Somaliawalio kwenye mazingira magumu nchini humo baada ya kushindwa kuendelea na safari ya ughaibuni.

Msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe amesema ombi la awali la dola Milioni 72 kwa Djibouti kupitia mchakato wa Umoja wa Mataifa bado halijatekelezwa na sasa wanahitaji haraka fedha hizo kukwamua wahamiaji hao walio kwenye ofisi ya IOM huko Obok nchini humo.

Boda boda zaendelea kukatiza uhai wa watu kwenye ajali barabarani

Ni hivi  karibuni tu shirika la afya duniani WHO lilitoa ripoti  inayoonesha kuwa ni mataifa 28 pekee yenye asilimia 7 ya watu wote duniani yana sheria madhubuti za usalama barabarani kwenye maeneo makuu matano ambayo ni kunywa pombe na kuendesha gari, mwendo kasi kupindukia, matumizi ya kofia kwa waendesha pikipiki, kufunga mikanda na matumizi ya viti maalum kwa watoto.

Unicef yapiga kambi Niger kukabiliana na utapiamlo

Mapigano yanayoendelea nchini Mali yamesababisha zaidi ya wakazi 270,000 wa nchi hiyo iliyoko Magharibi mwa Afrika kukimbilia nchi jirani kutafuta hifadhi. Hata hivyo wakiwa njiani wanakumbana na kadhia mbalimbali na watoto wa wanawake huathirika zaidi.  Nchini Niger, ambako yanapokelewa makundi ya wakimbizi kutoka Mali, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limelazimika kupiga kambi humo kusaidia kwa matibabu kutokana na magonjwa kadhaa, ukiwemo utapiamlo unaotokana na lishe duni. Basi kupata undani wa ripoti hiyo ungana na Joseph Msami.

Surua yatishia usalama wa watoto DRC Kongo,UNICEF yasaidia

Mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC pamoja na mambo mengine yametajwa kukwamisha jitihada za kukabiliana na hatimaye kudhibiti ugonjwa wa surua hususani mongoni mwa watoto.Hii inatokana na kwamba mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi yamesababisha watu kukimbia makazi yao na kuishi katika makzi yenye msongamano .Jitihada za kutoa chanjo zinakwama!