Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasaidia wahanga wa mafuriko Zimbabwe

IOM yasaidia wahanga wa mafuriko Zimbabwe

Pakua

Mvua kubwa zilizoanza kunyesha katikati ya mwezi huu huko Zimbabwe zimesababisha mafuriko ambayo yameharibu miundombinu ya kijamii na kiuchumi ikiwemo barabara na shule.

Maelfu ya watu kwa sasa hawana makazi na wanahitaji msaada ambapo shrika la kimataifa la uhamiaji, IOM, kwa kushirikiana na idara ya ulinzi wa raia nchini Zimbabwe wameitikia wito wa kutoa misaada kwa wahanga wa mafuriko hayo.

Jumbe Omari Jumbe wa IOM akizungumza na Radio ya UM amesema  kuwa maeneo yaliyoathirika zaidi ni majimbo ya Matebele Kusini na Kaskazini, Manicaland, Mashonaland Kati, Masvingo na Midlands.