Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

05 OKTOBA 2022

Hii leo kwenye Habari za UN  tunamulika masuala ya amani na usalama, hali ngumu ya uchumi Tunisia yasababisha wananchi kutojua la kufanya, siku ya walimu duniani na uboreshaji wa madarasa huko Malawi.

1. Idadi kubwa ya matukio ya utesaji katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) vinatokea katika maeneo yaliyoathiriwa na mizozo ambako hali ya kutoadhibiwa kwa wahalifu imeenea.

Sauti
12'5"

04 OKTOBA 2022

Karibu kusikiliza jarida ambapo leo utasikia mada kwa kina inayomulika ni kwa vipi mashambulizi ya kikundi cha waasi cha M23 yanavuruga maisha ya wakazi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. 

Pia utapata kusiliza habari kwa ufupi ikiwemo ile inayohusu wakazi wa Jimbo la Cabo Delgado lililoko kaskazini mwa Msumbiji ambao wanatimiza miaka mitano tangu vurugu kuibuka katika eneo hilo na kusababisha zaidi ya watu milioni moja kuyakimbia makazi yao. 

Na mashinani utamsikia kijana mchechemuzi wa masuala ya elimu kutoka nchini Tanzania. 

Sauti
12'5"

30 SEPTEMBA 2022

Hii leo katika Habari za UN Flora Nducha anamulika:

Taarifa ya kwamba hatua za kutokomeza ubaguzi dhidi ya watu wenye asili ya Afrika zinatekelezwa vipande vipande licha ya harakati zinazoendelea za kuondokana na ubaguzi wa kimfumo.

Nchini Ureno ,shirika moja lililoanzishwa na Maria Ramires linasaidia wanawake wazee kujijengea mnepo hata wakati wa utu uzima, mathalani kujifunza kuendesha merikebu zenye matanga.

Sauti
10'39"

29 SEPTEMBA 2022

Hii leo Alhamisi ni mada kwa kina Flora Nducha anakupeleka nchini Kenya hususan kaunti ya Migoro kumulika changamoto ya elimu hasa maeneo ya vijijini, lakini zaidi ya yote ni kwa vipi elimu sio tu ufunguo wa maisha bali pia msingi wa maendeleo kama usemavyo Umoja wa Mataifa.

Habari wa Ufupi zinamulika ripoti kuhusu nchi 42 kubinya watu kushirikiana na Umoja wa Mataifa kwa kuwapatia vitisho au kulipa visasi. Halikadhalika siku ya kimataifa ya upotevu wa chakula kuanzia shambani hadi mezani na bila kusahau siku ya kimataifa ya usaifirishaji baharini.

Sauti
11'55"

28 SEPTEMBA 2022

Katika Habari za UN hii leo Flora Nducha anaanza na Afya ya akili miongoni mwa wafanyakazi na changamoto zake. Taarifa hii  kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwemo lile la afya ulimwenguni, WHO na ajira ILO. Mashirika yanasema ubaguzi, ukosefu wa usawa na unyanyasaji pahala pa kazi ni tatizo. Pili anakwenda Zambia kuona jinsi vituo vya maendeleo ya awali ya mtoto, ECD vimeleta tofauti chanya katika makuzi ya watoto.

Sauti
11'31"

27 Septemba 2022

Hii leo katika Habari za UN Flora Nducha anakuletea Habari kwa Ufupi, Mada kwa kina na Mashinani.

Katika Habari kwa ufupi: Kurejea nyumbani kwa hiyari kwa wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kutoka nchini Zambia. Pili kutangazwa kutokomezwa kwa EBola nchini DRC na Habari ya Tatu ni kuhusu siku ya utalii duniani na wito kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kutaka utalii wa aina mpya usioaharibu mazingira na wenye mnepo kwa kila mkazi wa dunia.

Sauti
13'48"

26 SEPTEMBA 2022

Hii leo kwenye Habari za UN Flora Nducha anaanza na Sudan Kusini ambako wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu nchini humo wanataka jamii ya kimataifa itupie jicho la umakini mkataba wa amani wa mwaka 2018 ili uweze kutekelezwa kwa umakini, kwani hivi sasa kuna shaka na shuku ya utekelezaji wake kikamilifu. Kisha ni nchini Tanzania ambako shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limezindua mradi wa thamani ya zaidi ya dola milioni 9 ili kuimarisha usalama wa mazao. Makala ni kijana mkimbizi kutoka Sudan Kusini ambaye sasa anaishi Canada.

Sauti
12'51"

23 SEPTEMBA 2022

Hii leo kwenye Habari za UN, Flora Nducha anaanza na taarifa kutoka ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambako Rais wa mpito nchini Burkina Faso Paul Damiba anaelezea hatua walizochukua kurejesha utulivu nchini mwao.

Kisha anakwenda Turkana nchini Kenya ambako mtoto  Carol mwenye umri wa miaka 11 alinajisiwa na mzee ambaye alikuwa amuoe kwa lazima lakini tukio hilo lilisambaratishwa na wapasha  habari, sasa anaelekea kutimiza ndoto yake ya shule.

Audio Duration
11'38"

22 SEPTEMBA 2022

Hii leo katika Habari za UN Flora Nducha anakuletea mada kwa kina, Habari kwa Ufupi na Neno la Wiki.

Habari kwa Ufupi zinamulika harakati za kutumia chanjo inayoweza kukabili virusi aina ya #EbolaSudan nchini Uganda kwa kuwa chanjo ya sasa haina uwezo huo. Pia nafasi ya nishati jadidifu katika kuongeza ajira duniani, ripoti mpya imethibitisha hilo! Kisha wito wa Rais wa Botswana kwenye mjadala mkuu wa UNGA77 wa kutaka wananchi wake nao waajiriwe Umoja wa Mataifa.

Sauti
12'36"