Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

05 OKTOBA 2022

05 OKTOBA 2022

Pakua

Hii leo kwenye Habari za UN  tunamulika masuala ya amani na usalama, hali ngumu ya uchumi Tunisia yasababisha wananchi kutojua la kufanya, siku ya walimu duniani na uboreshaji wa madarasa huko Malawi.

1. Idadi kubwa ya matukio ya utesaji katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) vinatokea katika maeneo yaliyoathiriwa na mizozo ambako hali ya kutoadhibiwa kwa wahalifu imeenea.

2. Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limesema wananchi wengi wa Tunisia hivi sasa wanakabiliwa na machaguo magumu ya kubaki ndani ya nchi yao na kukabiliwa na hali ngumu ya maisha na uhaba wa chakula au kukimbia nje ya nchi yao na kutojua nini kitatokea huko waendako.

3. Makala: Mwalimu nchini Tanzania atumia mbinu bunifu kupatia wanafunzi stadi za kujifunzia badala ya kukosa vifaa vya kisasa.

4. Mashinani tunakwenda Malawi, mwanafunzi anatoa shukrani kwa UNICEF kwa kuwapatia madawati mapya. Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.

Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Sauti
12'5"