Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

28 Februari 2022

karibu kusikiliza jarida na kama ilivyo ada kila Jumatatu tunakuletea mada kwa kina, mahojiano maalumu na mmoja wa waliokuwa ngariba nchini Tanzania lakini sasa ameacha shughuli hiyo ya ukeketaji baada ya kuelimika.

Pia Flora Nducha atakuletea habari kwa ufupi kubwa likiwa ni mapigano nchini Ukraine na namna Umoja wa Mataifa unavyoshughulikia.

 

Sauti
14'53"

28 Februari 2022

karibu kusikiliza jarida na kama ilivyo ada kila Jumatatu tunakuletea mada kwa kina, mahojiano maalumu na mmoja wa waliokuwa ngariba nchini Tanzania lakini sasa ameacha shughuli hiyo ya ukeketaji baada ya kuelimika.

Pia Flora Nducha atakuletea habari kwa ufupi kubwa likiwa ni mapigano nchini Ukraine na namna Umoja wa Mataifa unavyoshughulikia.

 

Sauti
14'53"

25 FEBRUARI 2022

Karibu kusikiliza jarida ikiwa leo ni siku ya mada kwa kina kunaelekea nchini Uganda kuangazia kwa undani athari  za kiuchumi za mafuriko ambayo yamedumu kwa miaka miwili sasa kwa wakazi hasa wa ziwa Albert baada ya kusababisha hasara kubwa ya mali.

Pia utasikia habari kwa ufupi zikisomwa na Flora Nducha na kubwa ni kuhusu msaada wa kibinadamu kwa wananchi wa Ukraine pamoja na Madagascar. 

Sauti
12'58"

24 Februari 2022

Karibu kusikiliza jarida ambapo miongoni mwa utakayo yasikia hii leo ni pamoja na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yameeleza madhara yanayotokea hususan kwa watoto nchini Ukraine kutokana na mashambulizi. Mathalan shirika la Umoja wa Mastaifa la kuhudumia Watoto UNICEF limesema linatiwa wasiwasi mkubwa kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi ambayo yanatoa tishio kubwa kwa maisha na ustawi wa Watoto milioni 7.5 nchini humo.

Sauti
12'26"

23 Februari 2022

Karibu kusikiliza jarida ambapo leo tutakuletea mada kwa kina kutoka viziwani Zanzibar nchini Tanzania , ambapo ikiwa imesalia chini ya miaka 8 kufikia ukomo wa malengo ya amendeleo endelevu SDG’s juhudi zinafanyika kwa hali na mali kuhakikisha jamii zinafikia malengo hayo. Miongoni mwa wanaharakati wa kupigia upatu malengo hayo ni mke wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Bi. Mariam Mwinyi ambaye mwishoni mwa wiki amezindua wakfu au taasisi maalum ijulikanayo kama “Zanzibar Maisha Bora Foundation”.

Sauti
15'32"

22 Februari 2022

Karibu kusikiliza jarida ambapo leo miongoni mwa utakayosikiani pamoja na ziara ya Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean Pierre Lacroix nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC, kumuwakilisha Katibu Mkuu.

Naibu mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa na mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Somalia, Adam Abdelmoula, ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuzisaidia haraka jamii zilizoathirika vibaya na ukame baada ya kukamilisha ziara ya siku mbili katika maeneo yaliiyoathika zaidi Somaliland.

Sauti
13'23"

21 Februari 2022

Leo ni siku ya kimataifa ya lugha mama. Lugha mama ni ile ambayo mtu anaizungumza ya kwanza na inaweza kuwa pale alikozaliwa au ni lugha ya asili ya jamii yake. Kwa wengi wa wakazi wa nchi za Afrika Mashariki, Kiswahili ni lugha mama kwa kuwa inazungumzwa katika nchi zote za eneo hilo na zile za jirani na pia ni lugha ya kufundushia shuleni. Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni, UNESCO linasema maudhui ya mwaka huu ya siku hii ni matumizi ya teknolojia katika kujifunza lugha mbalimbali, fursa na changamoto.

Sauti
12'15"

18 FEBRUARI 2022

Katija Jarida la mada kwa kina hii leo kutoka Umoja wa Mataifa KLeah Mushi anakuletea

-Malawi imetangaza kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa polio nchini humo na hivyo kuwa ni tangazo la kwanza la uwepo wa ugonjwa huo barani Afrika katika kipindi cha zaidi ya miaka mitano. 

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linashirikiana na mamlaka nchini Ethiopia na wadau wake kupatia msaada wa dharura kwa maelfu ya wakimbizi kutoka Eritrea ambao walikimbia kambi ya Barahle na viunga vyake huko jimboni Afar baada ya mapigano kuibuka eneo hilo. 

Sauti
10'36"

17 Februari 2022

Hii leo tunaanzia Ukanda wa Sahel ambako wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa yameshuhudia wakimbizi wakishiriki kwenye miradi ya kilimo na ujenzi wa nyumba ili kujipatia kipato. Kisha tunabisha hodi huko nchini Tanzania kumulika mradi wa uvuvi usioharibu mazingira unaotekelezwa na na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO kupitia mradi wa FISH4ACP. Habari nyingine ni kuhusu tamasha la amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC huko mjini Goma jimboni Kivu Kaskazini.

Sauti
13'23"