Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

29 SEPTEMBA 2022

29 SEPTEMBA 2022

Pakua

Hii leo Alhamisi ni mada kwa kina Flora Nducha anakupeleka nchini Kenya hususan kaunti ya Migoro kumulika changamoto ya elimu hasa maeneo ya vijijini, lakini zaidi ya yote ni kwa vipi elimu sio tu ufunguo wa maisha bali pia msingi wa maendeleo kama usemavyo Umoja wa Mataifa.

Habari wa Ufupi zinamulika ripoti kuhusu nchi 42 kubinya watu kushirikiana na Umoja wa Mataifa kwa kuwapatia vitisho au kulipa visasi. Halikadhalika siku ya kimataifa ya upotevu wa chakula kuanzia shambani hadi mezani na bila kusahau siku ya kimataifa ya usaifirishaji baharini.

Leo kwenye Jifunze Kiswahili, Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar ,BAKIZA anafafanua msemo “ndege asili ya Buga kufugwa hawezekani, atenda tafuta Boga japo Tama li Bandani,” karibu!

Audio Credit
FLORA NDUCHA
Audio Duration
11'55"