Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

28 Juni 2022

Karibu kusikiliza jarida ambapo wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari ukiendelea mjini Lisbon, Ureno kujadili suluhu za kukabiliana na changamoto za bahari tunakuleta mada kwa kina ikimulika eneo la Vanga Kilifi huko Kenya wanachi wamepata moja ya suluhu kubwa ambayo ni kuvuna na kuuza hewa ukaa kutoka kwenye mikoko kupitia mradi wa Vanga Blue Forest VBF, ambao kwa kiasi fulani unafadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP. 

Sauti
11'40"

27 Juni 2022

Hii leo jaridani, Anold Kayanda anaanzia Ureno kwenye mkutano kuhusu bahari ambako Umoja wa Mataifa unasema kama taka za plastiki hazidhibitiwi, basi taka hizo zitakuwa nyingi kuliko samaki ifikapo mwaka 2050. Kisha anasalia huko huko kwake Nancy Iraba mwanasayansi wa masuala ya bahari kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam nchini Tanzania akizungumzia vijana na ubunifu katika kulinda bahari. Makala anakwenda Kenya kusikia mnufaika wa kilimo cha mwani. Na mashinani anasalia Ureno.
Sauti
10'31"

24 Juni 2022

Hii leo jaridani, Leah Mushi anamulika:
1.    Chuo cha sanaa Kivu, AKA huko Goma jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na harakati za kutumia uchoraji wa kuta ili kuepusha vijana na ghasia sambamba na kulinda mazingira.
2.    Nchini Mauritania IFAD imeleta nuru kwa wakulima waliokosa mvua
3.    Makala tunakwenda Kigali, Rwanda kwenye mkutano wa viongozi wa nchi za Jumuiya ya Madola ambako kijana Paul Siniga kutoka Tanzania amewakilisha vijana.

Sauti
11'49"

22 Juni 2022

Hii leo katika jarida utasikia kuhusu tetemeko kubwa la ardhi lililoyakumba majimbo mawili nchini Afghanistan, tayari serikali ya Taliban imeomba msaada kwa Shirika la Umoja wa Mataifa. - Umoja wa Mataifa na mashirika mengine yanajiandaa kupelekea misaada ya kibinadamu nchini humo. Shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO Barani Afrika whapo kesho watakuwa na mkutano wa dharura ili kuanngalia iwapo ugonjwa wa homa ya nyani au Monkeypox nijanga la afya ya umma au la.
Sauti
11'33"

21 Juni 2022

Hii leo jaridani Leah Mushi anakuletea Mada kwa Kina inayotoka huko nchini Uganda kwake John Kibego ambaye amevinjari na kuzungumza na wakimbizi kuhusu simulizi za kule walikotoka na waliko hivi sasa .Mazingira yako vipi? Mmoja anasema, "tulichoshwa na vitendo vya kubakwa." Pia kuna habari kwa ufupi ikiangazia ongezeko la idadi ya watu wanaosaka hifadhi katika nchi ya tatu; sakata la elimu kwa watoto wanaoishi kwenye maeneo ya mizozo na pia uzinduzi wa apu ya kumwezesha mtu kufahamu wakati wa kutumia mafuta ya kuepusha mionzi mikali ya jua mwilini. Karibu!

Sauti
11'37"

20 Juni 2022

Jarida hii leo linajikita na siku ya wakimbizi ambapo mwenyeji wako Leah Mushi anaanza na ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ya kwamba kusaka hifadhi ni haki ya msingi ya kila binadamu. Kisha anakupeleka Canada jimboni Nova Scotia ambako wakimbizi kutoka kambini Kakuma nchini Kenya siyo tu wamepata hifadhi bali pia wameajiriwa kupitia mpango maalum wa UNHCR, serikali ya CANADA na shirika la kiraia la kupatia ajira wakimbizi kwenye stadi. Makala ni Iran huko ambako mradi wa kupatia bima wakimbizi umeleta ahueni kwa familia ya mkimbizi mwenye mahitaji makubwa kiafya.

Sauti
9'57"

17 Juni 2022

Hii leo Ijumaa, Leah Mushi anakuleta jarida la habari likimulika: 
1.    Watoto kutawanywa duniani kote kutokana na machafuko, taarifa kutoka UNICEF 
2.    Mhamasishaji wa kijamii atumia ngoma na kipaza sauti kuhamasisha wazazi na walezi kupeleka watoto wao kupata chanjo. 
3.    Makala anakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako Byobe Malenga amemulika utumikishaji watoto jimboni Kivu Kusini. Mtoto katoa ushuhuda. 

Audio Duration
11'23"

16 Juni 2022

Katika Habari kwa Ufupi Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO limesema bara la Afrika linaimarisha kasi ya utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 miongoni mwa watu walio hatarini zaidi na dalili zinaonesha mwelekeo ni mzuri. ===== Wafanyakazi wa majumbani licha ya umuhimu wa mchango wao katika jamii wa kutoa huduma ya malezi kwa familia na kaya kwa ujumla, bado wanasalia kutothaminiwa, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO. ==== Na kufuatia wito wa wataalamu wa Umoja wa MAtaifa wa haki za binadamu wa kutaka Tanzania isitishe zoezi la kile kinachodaiwa kuwa kumega
Sauti
13'40"