Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

30 SEPTEMBA 2022

30 SEPTEMBA 2022

Pakua

Hii leo katika Habari za UN Flora Nducha anamulika:

Taarifa ya kwamba hatua za kutokomeza ubaguzi dhidi ya watu wenye asili ya Afrika zinatekelezwa vipande vipande licha ya harakati zinazoendelea za kuondokana na ubaguzi wa kimfumo.

Nchini Ureno ,shirika moja lililoanzishwa na Maria Ramires linasaidia wanawake wazee kujijengea mnepo hata wakati wa utu uzima, mathalani kujifunza kuendesha merikebu zenye matanga.

Makala inabisha hodi Morogoro, mashariki mwa Tanzania ambako Chama cha Watu wenye Ualbino, TAS kinapita shuleni kuelimisha wanafunzi juu ya haki za watu wenye ualbino kama njia mojawapo ya kujenga utangamano kwenye jamii na kundi hilo.

Mashinani  ni wito wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO kwa wahudumu wa afya  pale watakapokuwa wanamtibu mgonjwa ambaye ni muathirika wa utumikishwaji haramu ya binadamu kama njia mojawapo ya kudhibiti usafirishaji haramu wa binadamu.

Audio Credit
FLORA NDUCHA
Audio Duration
10'39"