Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

31 Mei 2022

Jaridani Jumanne Mei 31, 2022 na Leah Mushi-

HABARI KWA UFUPI

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO leo limetoa taarifa mpya kuhusu kiwango ambacho tumbaku inaharibu mazingira na afya ya binadamu, ikitaka hatua zichukuliwe ili kuifanya sekta hiyo kuwajibikia zaidi juu ya uharibifu inayosababisha.

Sauti
13'16"

27 Mei 2022

Jaridani Mei 27, 2022

-Azimio la kulinda waandishi wa habari litekelezwe

-Mashujaa watanzania wawili miongoni mwa waliotunukiwa medali ya Dag Hammarskjold

Makala tunaangazia majukumu mengine yanyotekelezwa na walinda amani hususan nchini DRC

Mashinani ni ujumbe wa Mkuu wa Operesheni za ulinzi wa amani, kwenye Umoja wa Mataifa,  Jean-Pierre Lacroix. na wito wake kuelekea siku ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila Mei 29.

Sauti
11'37"

26 Mei 2022

Jaridani Mei 26-2022 na Leaha Mushi

-Hafla maalum ikiongozwa na Katibu Mkuu Guteress yafanyika kwenye makao makuu kuwaenzi walinda amani wa Umoja wa Mataifa

-Walinda amani kadhaa waenziwa kwenye Umoja wa Mataifa kwa tuzo

-Na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF imeeleza kusikitishwa na vifo vya takriban watoto 11 wachanga waliozaliwa hivi karibuni, kufuatia moto katika kitengo cha watoto wachanga cha hospitali ya Tivaouane nchini Senegal. 

Mada kwa kina inaangazia walinda amani wa Umoja wa Mataifa walioko MONUSCO nchini DRC

Sauti
13'57"

25 Mei 2022

Jaridani Jumatano Mei 25, 2022 na Leah Mushi

-Umoja wa Mataifa utaendelea kusimama na Afrika asema Katibu Mkuu Antonio Guteress katika kuadhimisha siku ya Afrika.

-Mlinda amani wa Zimbabwe ashinda tuzo ya UN ya  mtetezi bora mwanajeshi wa masuala ya jinsia 2021

-Katika makal tutasikia mengi kuhusu ulinzi wa amani nchini Mali kupitia ujumbe wa kuweka utulivu nchini humo, MINUSMA

Mashinani tunakutana na Luteni Ndeye Sanou DIEYE mlinda amani katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA 

Sauti
12'15"

23 Mei 2022

Jaridani Jumatatu Mei 23, 2022 na Leah Mushi-

-UNHCR: Mzozo wa Ukraine na mingineyo imepelekea watu milioni moja kukimbia makwao

-Wakulima wa Embu Kenya wavalia njuga vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kwa kupanda miti:IFAD 

-Katika makala ni mwanamke shuhuda kwamba ugonjwa wa Fistula una tiba.

Mashinani ni ujumbe wa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu wahamiaji ulimwenguni

Sauti
16'54"

20 Mei 2022

FAO yasaidia wananchi wa Yemen kurejea kwenye ufugaji nyuki wa asili.

Mradi wa Sola wa UNICEF watatua changamoto za waathirika wa ukame Kori Ethiopia.

Makala imeangazia mmoja wa wafanyabiashara wadogo katika makao makuu ya Tanzania, Dodoma ambaye ni miongoni mwa wanaolamba shubiri ya athari za vita kati ya Urusi na Ukraine ambavyo vimesababisha athari ya kiuchumi duniani.

Mashinani ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na wito wake wa kulindwa kwa wahamiaji kwa ajili ya kuhakikisha usalama wao.

Sauti
11'40"

19 Mei 2022

Jaridani Alhamisi, Mei 19, 2022 na Leah Mushi kuanza nia habari kwa ufupi, kisha mada kwa kina na kumaliza na neno la wiki.

Watu milioni 59.1 walilazimika kukimbia makwao nchini mwao mwaka 2021 kwa mujibu wa ripoti yiliyotolewa leo kuhusu wakimbizi wa ndani GRID na kituo cha kimataifa cha kufuatilia uhamishwaji wa watu kilicho chini ya shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM.. Hii ni  ongezeko la watu milioni 4 zaidi kufikia mwishoni mwa mwaka 2021 ikilinganishwa na kipindi hicho mwaka 2020. 

Sauti
10'41"

18 Mei 2022

Jaridani Jumatano Mei 18, 2022 na Leah Mushi

-Joto laendelea kuongezeka duniani kwa mwaka wa 7 mfululizo: WMO

-Mkutano wa kirafiki wakutanisha walinda amani kutoka Tanzania na baadhi ya viongozi viongozi mashariki mwa DRC

-Katika makala tunaelekea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuungana na Mwandishi wetu wa huko Byobe Malenga akiangazia matumizi ya mitandao ya kijamii miongoni mwa wakimbizi katika kambi ya Lusenda.

-mashinani  tutasikia kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP.

Sauti
13'30"

17 Mei 2022

Jaridani na Leah Mushi-

HABARI KWA UFUPI 

Idadi ya watoto walioathirika na uzito mdogo wa kupindukia imekuwa ikiongezeka hata kabla ya viya ya Ukraine ambayo inatishia kuitumbukiza dunia kwenye mgogoro mkubwa wa chakula imeonya ripoti mpya kuhusu watoto iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. 

==============================================================================================

Sauti
12'6"