Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

Jarida 31 Januari 2022

Miongoni mwa tuliyonayo kutoka Umoja wa Mataifa 

Wakimbizi wa Burundi walioishi kwa vipindi tofauti na hata miongo kadhaa ukimbizi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kwa msaada wa shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR wameanza kurejea nyumbani Burundi. Kundi la kwanza katika mwaka huu wa 2022 waeleza furaha yao kurejea nchini mwao.  

Sauti
10'40"

Jarida 28 Januari 2022

Miongoni mwa tuliyonayo hii leo 

Jamii ya Maasai tarafa ya Liliondo, Wilayani Ngorongoro katika mkoa wa Arusha kaskazini mwa Tanzania waanza kuamia katika shughuli ngeni kwao, kilimo baada ya shughuli yao ya kitamaduni yaani ufugaji, kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi. 

Sauti
10'34"

Jarida 26 Januari 2022

Miongoni mwa tuliyonayo


Mwenyekiti wa Bodi ya Ubia wa Elimu Duniani, GEP, Jakaya Kikwete azungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kueleza wanachofanya kuboresha mifumo ya elimu duniani. Ni baada ya kukutana na  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kwa lengo la kujadili mustakabali wa mifumo ya elimu kwa nchi maskini.

Sauti
12'15"

Jarida 25 Januari 2022

Miongoni mwa tuliyonayo katika habari za Umoja wa Mataifa


Familia za wakimbizi wa ndani pamoja na zile zilizowakaribisha wakimbizi hao katika ukanda wa mashariki ya kati kwa sasa zinakabiliana na baridi kali kutokana na kuanguka kwa theluji wakati huu wanaishi kwenye mahema.

Sauti
12'54"

Jarida 24 Januari 2022

Miongoni mwa tuliyonayo katika habari za Umoja wa Mataifa 


Ikiwa leo ni siku ya elimu duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema janga la COVID-19 na changamoto nyingine zinazokabili dunia hivi sasa zimedhihirisha umuhimu wa kurekebisha mfumo wa elimu ili uweze kukidhi mahitaji ya sasa.


Wakati huo huo Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF limesema kiwango cha hasara wanayopata watoto kielimu kutokana na kuvurugika kwa mfumo wa elimu kulikosababishwa na ugonjwa wa COVID-19 ni vigumu kurekebishika.

Sauti
11'44"

Jarida 21 Januari 2022

Machache kati ya mengi kutoka Umoja wa Mataifa  

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amelihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani na kutaja maeneo makuu matano ya vipaumbele vyake ambayo yanahitaij hatua za dharura ili kuweza kukabili changamoto zinazokabili Dunia hivi sasa. Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Profesa Kennedy Gastorn anachambua maana ya tukio hili. 

Sauti
10'50"

Jarida 20 Januari 2022

Miongoni mwa tuliyonayo hii leo kutoka Umoja wa Mataifa 

Programu ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA kufundisha masuala ya haki za binadamu katika shule za watoto wakimbizi wa kipalestina katika ukanda wa Gaza, imesaidia siyo tu wanafunzi kutambua haki zao bali pia walimu ambao wanawafundisha na hivyo kusaidia katika kusongesha amani kwenye eneo ambalo hugubikwa na migogoro. 

Sauti
12'4"

Jarida 19 Januari 2022

Kama ilivyo ada ya kila Jumatano tunakuletea mada kwa kina ambapo leo tunaangazia namna mradi wa mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD, ulivyogeuza maskini wa mjini huko Misri kuweza kukimu maisha vijijini kwa staha. 

Katika habari nyingine, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Abdullah Shahid ametoa hotuba yake ya vipaumbele vya kazi kwa mkutano huo wa 76 wa Baraza Kuu ambapo ametaja vipaumbele vikuu vitano vya kutekeleza katika mwaka huu 2022.  

Sauti
9'52"

Jarida 18 Januari 2022

Baadhi ya tulionayo hii kutoka Umoja wa Mataifa 

Nchini Afghanistan, majira ya baridi kali yamebisha hodi huku wakimbizi wa ndani waliosaka hifadhi kwenye mji mkuu Kabul wakihaha kujikinga na familia zao kwenye mahema yasiyo na vifaa vya kuleta joto. 

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la masuala ya Kiuchumi na Kijamii, ECOSOC Collen Vixen Kelapile ameiteua Tanzania kuwa Mwenyekiti Mwenza wa Jukwaa la Saba la Wadau Mbalimbali wa masuala ya Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi katika kutekeleza Agenda 2030 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa. 

Sauti
14'54"