Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

31 AGOSTI 2022

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea 

-Leo ni siku ya kimataifa ya watu wenye asili ya Afrika, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anasema licha ya mchango wao mkubwa bado wanaendfelea kubaguliwa kote duniani.

-Meli iliyosheheni msaada wa chakula kilichonunuliwa na shirika la mpango wa chakula duniani WFP kutoka nchini Ukraine kwenda Ethiopia imetia nanga jana nchini Djibout tayari kusambazwa kwa msaada huo

Sauti
10'50"

30 AGOSTI 2022

Katika jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea 

-Nusu ya vituo vya huduma za afya duniani kote vinakosa huduma za usafi na hivyo kuwaweka wagonjwa na wahudumu wa afya katika hatari kubwa ya kusambaza magonjwa na maambukizi kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo na WHO na UNICEF.

Sauti
12'56"

29 AGOSTI 2022

Flora Nducha anakuletea jarida lililo sheheni habari mbalimbali kuanzia nchini Ethiopia ambapo tume ya Kimataifa ya wataalamu wa Haki za binadamu nchini Ethiopia imekasirishwa na kuzuka upya kwa uhasama kati ya serikali ya Ethiopia na chama cha Tigray People's Liberation Front tangu wiki iliyopita na kuzitaka pande zote mbili kurudi kwenye meza ya mazungumzo kwani wanaoteseka ni raia.

Wakimbizi wa Burundi wakioko katika kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma nchini Tanzania wameshukuru kwa watoto wao kupatiwa vyeti vya kuzaliwa 

Sauti
10'26"

26 AGOSTI 2022

Katika Jarida la habari za UN hii leo Flora Nducha anakuletea -Mradi wa maji safi na salama jimboni Cibitoke nchini Burundi kwa msaada wa UNICEF umeleta afuweni kwa wakazi na hasa watoto -Mkimbizi kutoka DRC anayeishi Kakuma Kenya ameleta nuru ya nishati ya sola kwa wakimbizi wenzie huku akijiingizia kipato -Makala leo inatupeleka Tanzania kumulika jitihada za vijana katika kupambana na ukimwi na afya ya uzazi kwa kuelimisha vijana Balehe -Na mashinani afisa wa shirika la afya duniani WHO nchini Senegal anaeleza changamoto za upatikanaji wa taarifa za afya Afrika
Sauti
11'51"

25 AGOSTI 2022

Katika Jarida la Umoja wa Mataifa la mada kwa kina hii leo Flora Nducha anakuletea

-Ni miaka mitano tangu kuzuka kwa mgogoro wa Rohingya nchini Myanmar ambapo mamilioni walilazimika kufungasha virago na wengi kuingia nchini Bangladesh, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema takribani milioni 1 bado ni wakimbii na 150,000 wanaishi makambini Rakhine Bangladesh

Sauti
12'43"

24 AGOSTI 2022

Katika Jarida la habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea
-Ni miei sita tangu kuzuka kwa vita nchini Ukraine, mashirika ya Umoja wa Mataifa yamefanya nini hadi sasa kuwasaidia wananchi wa taifa hilo?
-Nchini Sudan Kusini mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani UNMISS umejenga shule na kituo cha polisi mjini Mvolo katika jitihada za ujenzi wa amani

Sauti
11'45"

23 AGOSTI 2022

Katika Jarida la habari la Umoja wa Mataifa hii leo , Flora Nducha anakuletea

-Mlipuko mpya wa Ebola wazuka Kivu Kaskazini baada ya mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 46 kufariki dunia na kuthibitishwa kuwa alikuwa na virusi vya Ebola kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO

Sauti
11'33"

22 AGOSTI 2022

Katika Jarida la habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Takribani watoto 1000 wameuawa au kujeruhiwa katika vita inayoendelea Ukraine UNICEF yatoa wito wa kusitisha uhasama na kuwalinda watoto hao

-Nchini Sudan Kusini katika eneo la Tamboura mafunzo yanayotolewa na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNMISS na shirika la ANIKA waleta nuru kwa wakazi

Sauti
12'23"

19 AGOSTI 2022

Hii leo jaridani tunamulika siku ya kimataifa ya usaidizi wa binadamu duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatoa shukrani kwa wale wote wanaojitolea kuchukua hatua kusaidia wengine hata wenyewe wakiwa bado na shida, huku akikumbuka wale waliopoteza maisha wakisaidia wengine. Tunakwenda pia Mexico huko ambako taka za mwani zinatengeneza matofali. Makala tunabisha hodi Kigoma, Leah Mushi anakuletea simulizi ya wanawake wanufaika wa miradi inayotekelezwa na UNDP chini ya KJP. Mashinani ni wito kutoka kwa Mkuu wa WHO ili kusaidia wakazi wa jimbo la Tigray nchini Ethiopia.

Sauti
11'48"

18 AGOSTI 2022

Hii leo jaridani tuna Habari kwa Ufupi ikianzia Ukraine ambako Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres yuko ziarani na anasema mashirika ya kiraia na taasisi za elimu ya juu ni muhimu zaidi hivi sasa kusongesha demokrasia ya kweli. Kisha tunakwenda Syria huko mtoto ameuawa na kilipuzi alichokuwa akichezea. Na hatimaye Zimbabwe wanaweke nyavu madirishani na milangoni kuzuia mbu.

Sauti
13'29"