Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

April 29 2022

Karibu kusikiliza jarida hii leo ambapo utapata fursa ya kusikiliza makala ya athari za Mafuriko kwenye sekta ya elimu nchini Uganda na kujifunza kiswahili, leo ufafanuzo wa methali Umejigeuza Pweza kujipalia Makaa umetolewa

 

Pamoja na hayo utapata fursa ya kusikiliza taarifa ya habari kwa ufupi ambapo

- Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO imefichua kiwango cha kushtua cha soko au uuzaji wa kinyonyaji wa maziwa ya mtoto yanayotegenezwa viwandani. 

Sauti
10'52"

28 Aprili 2022

Jaridani Alhamisi Aprili 28, 2022 na Leah Mushi

-Wasichana wanachohitaji ili kukumbatia ICT ni fursa na usalama mtandaoni: ITU 

-UNMISS kubadili mbinu za utoaji wa misaada ya kibinadamu Malakal

-UNICEF DRC yawezesha wanafunzi kujivunia shule yao

-Makala ni wito kwa serikali ya Tanzania kuuboresha mfumo wa ajira serikalini ili sera ya kuwajumuisha watu wenye ulemavu iweze kutekelezwa na watu kama yeye waweze kupata nafasi za ajira.

Mashinani ni ujumbe mahususi kutoka kwa Katibu Mkuu wa ITU.

Sauti
13'11"

26 Aprili 2022

Jaridani Jumanne Aprili 26, 2022 na Leah Mushi

-Usimamizi wa data ni muhimu ili biashara mtandao inufaishe wote- Naibu Katibu Mkuu Amina J. Mohammed.

Tani bilioni 50 za mchanga na changarawe hutumika kila mwaka duniani:UNEP

Mzozo wa wakulima na wafugaji Sudan Kusini wasababisha vifo vya zaidi ya watu 13.

Sauti
13'12"

25 Aprili 2022

Jarida la Jumatatu Aprili 25 kwanza ni habari kwa ufupi-

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) umelaani vikali unyanyasaji na ukatili wa kingono ulioenea, mauaji ikiwa ni pamoja na watu kukatwa vichwa, kuchomwa moto raia wakiwa hai, na mashambulizi dhidi ya wahudumu wa misaada ya kibinadamu katika Kaunti ya Leer.  

============================

Sauti
13'32"

22 Aprili 2022

Hii leo Jaridani mwenyeji wako ni Grace Kaneiya akikuletea jarida limesheheni mada kwa kina, Habari kwa Ufupi na kujifunza kiswahili.

Mada kwa kina ni uzinduzi wa filamu ya Royal  Tour Tanzania uliofanyika hapa Marekani na tunamulika mchango wake katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDG na mchambuzi ni Gerson Msigwa, Msemaji wa serikali ya Tanzania. 

Sauti
12'47"

21 Aprili 2022

Hii leo jaridani Grace Kaneiya anaanzia huko Ukraine ambako idadi ya wakimbizi wa ndani inazidi kuongezeka kutokana na vita vinavyoendelea. Kisha anakwenda Kenya kuona jinsi wafanyakazi wa kujitolea wa kijamii wameweza kushawishi wanajamii kukubali chanjo dhidi ya COVID-19. Atasalia huko huko Kenya ambako mashirika ya Umoja wa Mataifa yameleta nuru kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi kwa kuwapatia mradi wa umwagiliaji maji. Makala tunafunga safari hadi Brazili kuangazia maisha ya wahamiaji na wakimbizi ambao ni watu wa asili wa Warao kutoka Venezuela.

Sauti
13'18"

20 Aprili 2022

Hii leo jaridani na Grace Kaneiya ni mada kwa kina ikimulika harakati za taasisi ya TAI nchini Tanzania ya kutumia michezo ya kuigiza, vikaragosi, au katuni za kwenye majarida au zenye sauti kuelimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo haki, elimu na afya. Anold Kayanda amezungumza na Ian Tarimo, kiongozi wa taasisi hiyo ambaye alikuwa jijini New York, Marekani.

Sauti
13'28"

19 Aprili 2022

Karibu jaridani hii leo na Grace Kaneiya akianzia Uganda ambako UNICEF na serikali ya Iceland wamefanikisha  mradi wa kuhakikisha huduma ya maji safi na kujisafi (WASH) kwa wanafunzi wote kwenye shule za wilaya za Adjumani na Arua nchini Uganda. Kisha anabisha hodi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC huko serikali imepatia wakimbizi na wenyeji ardhi ya ekari 500 kuimarisha kujitegemea, mkimbizi katoa shukrani. Jarida linasalia huko huko DRC kumulika juhudi za UNICEF kuona watoto wanasoma licha ya kuishi kwenye vituo vya ukimbizini.

Sauti
12'51"

18 Aprili 2022

Hii leo katika Jarida la Habari tunamulika kwa kina ukame na njaa Pembe ya Afrika ambapo Msadizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Naibu Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya dharura, OCHA. Bi. Joyce Msuya anazungumzia kile ambacho wanafanya kusaidia wakazi wa eneo hilo. Habari kwa Ufupi inamulika chanjo ya Polio Ethiopia, uzinduzi wa kituo cha kimataifa cha tiba asilia nchini India na kumalizika kwa mzozo baina ya jamii a walendu na wahema huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, waliokuwa wakizozozana juu ya matumizi ya kanisa.

Sauti
12'31"