Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

29 JULAI 2022

Hii leo jaridani tunamulika pengo la huduma za ulinzi kwa wakimbizi na wasaka hifadhi wanapokuwa kwenye safari za kusaka maisha bora.  Ni ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR. Kisha tunabisha hodi Tanzania hususan mkoani Kigoma ambako shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO, limezindua Mtandao wa Wanawake Wanaojihusisha na Shughuli za Uvuvi TAWFA kupitia mradi wake wa kukuza mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi katika ziwa Tanganyika.

Sauti
13'54"

28 JULAI 2022

Leo ni siku ya homa ya ini duniani! Hivyo tunakuletea jarida maalum linaloangazia kwa undani aina, maambukizi na vipi mtu anaweza kujikinga asipate homa ya ini ambayo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO linasema zaidi ya wakazi milioni 91 barani Afrika wanaishi nao hususan aina B au C ambayo ni mbaya zaidi. WHO inasema iwapo homa ya ini haitagunduliwa mapema unaweza kupata saratani au kansa ya ini. Je kuna aina ngapi ya homa ya ini? Homa Kali ya ini ni ipi ambayo imegunduliwa sasa? Njia za maambukiz ini zipi? Na nini ufanye uweze kujikinga?

Sauti
14'2"

27 JULAI 2022

Hii leo jaridani tunaanzia huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako ghasia zinaendelea dhidi ya vituo vya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, walinda amani watatu wa UN wameuawa na watu zaidi ya 61 wamejeruhiwa.. Umoja wa Mataifa umetoa tamko. Kisha kuna hali ya uchumi duniani na makala tunakwenda Tanzania kumulika mbunifu wa gari la kutumia nishati  ya umeme, Ali Masoud ‘Kipanya’. Mashinani ni hali ya wanawake nchini Afghanistan, karibu na mwenyeji wako ni Assumpta  Massoi.

Sauti
14'18"

26 JULAI 2022

Hii leo jaridani Anold Kayanda anakuletea Habari kwa Ufupi; Mada Kwa Kina na Mashiani:

Katika Mada kwa Kina anasalia makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambako wiki iliyopita Naibu Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Amina J, Mohammed alizindua maonesho ya “Ulikuwa umevaa nini? Yakionesha nguo ambazo walivalia manusura wa ukatili wa kingono, kwa kuzingatia kuwa jamii humbebesha lawama ya kubakwa yule aliyebakwa badala ya aliyebakwa kwa kisingizio cha mavazi.

Sauti
12'24"

25 JULAI 2022

Hii leo jaridani tunaanza na siku ya kimataifa ya watu kuzama majini na Umoja wa Mataifa unataka hatua zaidi kuepusha watu kuzama majini kutokana na hali hiyo kuwa sababu inayoongoza kwa vifo vitokanavyo na ajali. Kisha tunabisha hodi Kenya ambako UNICEF inatoa wito kwa serikali itakayoingia madarakani kwenye uchaguzi mkuu ujao ipatie kipaumbele hifadhi ya jamii. Makala tunakwenda DRC kuona jinsi walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanatoa misaada kwa wanafunzi ili wajifunze Kiswahili na hatimaye wachangie katika kusongesha amani.

Sauti
11'33"

22 JULAI 2022

Hii leo jaridani kubwa ni kutiwa saini huko Istanbul Uturuki kwa makubaliano baina ya Urusi, Ukraine na Umoja wa Mataifa ya kuwezesha nafaka na vyakula kutoka Ukraine viweze kusafirishwa kupitia Bahari Nyeusi. Shuhuda wa Umoja wa Mataifa kwenye utiaji huo saini si mwingine bali ni Katibu Mkuu mwenyewe wa UN, Antonio Guterres.

Sauti
12'59"

21 JULAI 2022

Hii leo jaridani ni siku ya mada kwa kina, halikadhalika kuna Habari kwa Ufupi bila kusahau kujifunza lugha ya Kiswahili. Mada kwa kina inakupeleka Kaunti ya Migori nchini Kenya kumulika harakati za Umoja wa Mataifa kusaidia wakulima kuondokana na kilimo hatarishi cha tumbaku.

Sauti
10'46"

20 JULAI 2022

Hii leo katika jarida tunamulika doria zinazoendeshwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani Sudan Kusini, UNMISS jimboni Tambura, kisha sakata la kupungua kwa ukubwa wa chapati huko kambini Dzaleka nchini Malawi kutokana na COVID-19 na vita ya Ukraine kwa kuwa gharama za bidhaa zimeongezeka.

Sauti
12'53"

19 JULAI 2022

Hii leo jaridani tuna mada kwa kina mahsusi ikimulika raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC aitwaye Esperance Tabisha aliyenufaika na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuhamishia wakimbizi nchi ya tatu kupitia mkataba wa kimataifa wa wakmbizi, GCR. Katoka DRC kaingia kambini Kakuma nchini Kenya na kisha Canada na sasa ni mbunifu wa mitindo akitumia mtandao wa kijamii kupata wateja wake. Janga la COVID-19 lilikuwa chungu na tamu hapo hapo kwa vipi? Thelma anasimulia.

Sauti
12'5"

18 JULAI 2022

Hii leo jaridani tunamulika siku ya kimataifa ya Nelson Mandela kwa kukutelea ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuhusu nafasi ya hayati Mandela katika maendeleo na amani. Tunaangazia pia tamko la mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Haki ya Afrika wa kuamuru Kenya ilipe fidia jamii ya asili ya Ogiek kwenye msitu wa Mau. Makala ni mchezo wa kuigiza wa kushawishi wajawazito kwenda kliniki wakiwa na waume zao na Leah Mushi anakupeleka nchini Malawi.

Sauti
9'48"