Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

27 OKTOBA 2022

Hii leo jaridani ni Mada kwa Kina na tunakuunganisha moja kwa moja na mwenzetu Flora Nducha aliyeko Kigali nchini Rwanda akimulika harakati za shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, za kuhakikisha taifa hilo la Afrika Mashariki linatekeleza kwa ufanisi lengo namba 3 la malengo ya maendeleo endelevu, SDG la afya kwa wote na ustawi ifikapo mwaka 2030.

Hata hivyo kuna Habari kwa Ufupi na Leah Mushi akimulika:

Sauti
11'30"

25 OKTOBA 2022

Hii leo kwenye Jarida la Umoja wa Mataifa tunakuletea mada kwa kina ikimulika filamu ya chapa tatu iliyotengenezwa na taasisi ya Tai Tanzania kuhusu haki za binadamu yeyote yule wakiwemo watu wenye ualbino, Mtoto Njaro ana uwezo mkubwa wa ubunifu, anakutana na changamoto kwenye jamii yake lakini hakati tamaa, anasonga mbele hadi anaibuka mshindi.

Kuna habari kwa ufupi kutoka kwake Flora Nducha akimulika:

Sauti
12'48"

24 OKTOBA 2022

Hii leo Jarida la UN linamulika siku ya Umoja wa Mataifa ambao leo unatimiza miaka 77 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1945 huko Francisco nchini Marekani na kukuchambulia zaidi:

Sauti
13'

21 OKTOBA 2022

Hii leo jaridani Assumpta Massoi anaanzia Rwanda ambako Flora Nducha anafuatilia maadhimisho ya miaka 60 ya taifa hilo kwenye Umoja wa Mataifa, kisha anakwenda Tanzania ambako Stella Vuzo amemulika ziara ya Malkia Maxima wa Uholanzi ambaye ni Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ujumuishaji kifedha. Makala tunakwenda Zambia kumulika ni kwa vipi watoa huduma za kijamii wa kujitolea wanaepusha ndoa na mimba za utotoni.

Sauti
12'45"

20 OKTOBA 2022

Hii leo katika Jarida la Umoja wa Mataifa tuna Mada kwa Kina ikimulika harakati za kutokomeza ujinga wa kutokujua kusoma na kuandika kupitia elimu ya watu wazima au ngumbaru huko nchini  Kenya. Tayari wanufaika wameanza kuona matunda. Thelma Mwadzaya anakupitisha katika mtaa wa mabanda wa Kiambiu, huko Eastleigh jijini Nairobi.

Sauti
11'33"

19 OKTOBA 2022

Karibu kuungana na Assumpta Massoi anayekuletea jarida likiangazia masuala mbalimbali ikiwemo

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni limebainisha kuwa wagonjwa wa magonjwa yasiyo yakuambukiza kama vile utipwatipwa, kisukari na magonjwa ya moyo wanazidi kuongezeka duniani na serikali zitaingia gharama kubwa iwapo hazitaongeza nguvu katika kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi ya mwili.

Sauti
12'14"

18 OKTOBA 2022

Hii leo jaridani Assumpta Massoi anakuletea Mada Kwa Kina kuhusu harakati za Umoja wa Mataifa za kutokomeza umaskini kwenye mkoa wa Kigoma nchini Tanzania kupitia mashrika yake yanayotekeleza Mradi wa Pamoja wa Kigoma, KJP lakini pia kuna Habari kwa Ufupi zikimulika:

Sauti
11'43"