28 SEPTEMBA 2022
Katika Habari za UN hii leo Flora Nducha anaanza na Afya ya akili miongoni mwa wafanyakazi na changamoto zake. Taarifa hii kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwemo lile la afya ulimwenguni, WHO na ajira ILO. Mashirika yanasema ubaguzi, ukosefu wa usawa na unyanyasaji pahala pa kazi ni tatizo. Pili anakwenda Zambia kuona jinsi vituo vya maendeleo ya awali ya mtoto, ECD vimeleta tofauti chanya katika makuzi ya watoto. Makala anabisha hodi Tanzania ambako shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limegawa maziwa kwenye shule 4 za msingi mkoani Dodoma ikiwa ni siku ya kimataifa ya unywaji maziwa shuleni, na mashinani tunasalia hapa Umoja wa Mataifa kusikia ujumbe kutoka kwa kijana mchechemuzi wa haki kwa jamii na elimu kwa wote.