Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

30 NOVEMBA 2022

Jaridani leo tunaangazia mtandao wa intaneti barani Africa na juhudi za UNICEF Uganda katika shule moja ya msingi nchini humo. Makala tutaelekea nchini Tanzania Kusini Magharibi katika mkoa wa Mbeya na mashinani tutasalia hukohuko nchini Tanzania katika kambi ya wakambizi ya Nyarugusu.

Sauti
12'18"

29 NOVEMBA 2022

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina tukiangazia juhudi za kuwajengea watoto tabia ya kupenda kusoma vitabu na pia habari kwa ufupi zikiwemo ripoti ya UNAIDS na WHO, na usaidizi kwa wakimbizi na jamii za wenyeji nchini Chad. Mashinani tutakwenda nchini Cameroon, kulikoni?

Sauti
13'47"

28 NOVEMBA 2022

Hii leo jarida linakuletea habari za WHO na michuano ya fainali za Kombe la Dunia. Makala inatupeleka kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya kusikia simulizi ya msichana mnufaika wa mradi wa Girl Shine na Mashinani tutaelekea nchini Uganda kwa mkimbizi mwanaharakati wa mazingira

Sauti
10'56"

25 NOVENBA 2022

Hii leo jarida linaangazia afya nchini Haiti na ujenzi wa amani hasa kwa lengo la kuepusha vijana kutumbukizwa kwenye vikundi vyenye msimamo mkali huko Garissa nchini Kenya. Makala tunakwenda nchini Poland na Mashinani nchini Ethiopia, kuliko ni?  

Sauti
10'28"

23 NOVEMBA 2022

Hii leo jarida linamulika ukatili dhidi ya wanawake na wasichana na pia mradi wa kupatia fedha jamii nchini Malawi. Makala tunakwenda nchini Kenya na Mashinani nchini Tanzania.

Sauti
14'25"

22 NOVEMBA 2022

Hii leo jarida linaangazia Mada kwa kina tukimulika kongamano la kimataifa la wataalam wa kifua kikuu au TB lmjini Nairobi, Kenya na habari kwa ufupi ikiangazia kazi za Umoja wa Mataifa nchini Morocco, maandamano nchini Iran na walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.  Na mashinani tutaelekea Visiwa vya Solomoni katika eneo la kusini mwa Bahari ya Pasifiki, huko msemo wa "Majuto Mjukuu" umekuwa dhahiri,  kulikoni?

Sauti
12'5"

21 NOVEMBA 2022

Hii leo jarida linaangazia siku ya uvuvi, masuala ya watoto na makala tunakwenda nchini Somalia kumulika uhakika wa chakula kwa watu waliokumbwa na changamoto ya ukame na mafuriko, mashinani ni ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Sauti
12'29"

18 NOVEMBA 2022

Hii leo jarida linaangazia ripoti iliyotolewa leo na UNICEF kuhusu ubaguzi wa rangi na ubaguzi dhidi ya watoto na pia habari kutoka Garissa, Kenya, makala ya maandamanano ya wanaharakati huko Sharm-el-Sheikh nchini Misri kwenye mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa Mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP27, kisha mashinani nchini Ethiopia.

Audio Duration
12'15"

17 NOVEMBA 2022

Hii leo jaridani tunaangazia mada kwa kina na leo tunafunga safari hadi bara Hindi huko nchini India kusikia kuhusu kijiji cha kwanza nchini humo kinachotumia nishati ya sola pekee kwa wakazi wake zaidi ya 6,400.  Pia litakuletea Habari kwa ufupi kama zifuatayo:

Sauti
12'23"

16 Novemba 2022

Hii leo jaridani tunaangazia mabadiliko ya tabianchi na athari kwa wakimbizi, ziara ya afisa wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Makala tunamulika haki za wenye ualbino Uganda na mashinani tunamulika nafasi ya wananawake kwenye maamuzi.

Sauti
13'28"