Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

26 SEPTEMBA 2022

26 SEPTEMBA 2022

Pakua

Hii leo kwenye Habari za UN Flora Nducha anaanza na Sudan Kusini ambako wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu nchini humo wanataka jamii ya kimataifa itupie jicho la umakini mkataba wa amani wa mwaka 2018 ili uweze kutekelezwa kwa umakini, kwani hivi sasa kuna shaka na shuku ya utekelezaji wake kikamilifu. Kisha ni nchini Tanzania ambako shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limezindua mradi wa thamani ya zaidi ya dola milioni 9 ili kuimarisha usalama wa mazao. Makala ni kijana mkimbizi kutoka Sudan Kusini ambaye sasa anaishi Canada. Mashinani tunamulika mjadala mkuu wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa ujumbe wa Waziri Mkuu wa Samoa kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi hasa kwa nchi za visiwa vidogo. Karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
12'51"