Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Wakuu wa UM wanataka Wa-Kongo wasubiri matokeo rasmi

Likiwapongeza wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kushiriki katika uchaguzi wa kihistoria wa nchi yao, kwa sehemu kubwa kabisa kwa amani, siku ya Jumapili, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitoa mwito wiki hii kuwataka wawe watulivu na kusubiri matokeo ya mwisho ya uchaguzi.

Jaribio la Mapinduzi lagunduliwa Burundi

Afisi ya kulinda amani ya UM huko Burundi ONUB imeeleza kushangazwa na ripoti kua kulikuwepo na jaribio la kuipindua serekali ya Bujumbura, siku chache zilizopita na kwamba kuna wanasiasa mashuhuri walotiwa vizuizini.

UNICEF kulaani vitendo vya ubakaji wa watoto Zimbabwe

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF limelaani vikali sana habari za kutokea vitendo zaidi vya ubakaji huko Zimbabwe na likihimiza sheria mpya kupitishwa kuwalinda watoto wa nchi hiyo na kutoa masomo zaidi juu ya virusi vua HIV na Ukimwi.

Wafanyakazi wa kimataifa washindwa kuhudumia raia muhitaji katika jimbo la Sudan la Darfur

Shirika la UM juu ya Operesheni za Amani katika Sudan, UNMIS, limeripoti karibuni ya kuwa wafanyakazi wa kimataifa wanaosimamia huduma za kiutu katika Darfur wanakabiliwa na vizingiti vinavyokwamisha huduma za kuwasaidia raia kupata mahitaji ya kunusuru maisha kwa sababu ya kuendelea kwa mashambulio na hali ya utumiaji nguvu dhidi yao, pamoja na vitendo vya uharamia na mapigano yalioshtadi kati ya makundi ya waasi.~~