Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

FAO imechapisha mwongozo mpya kusaidia utetezi wa haki ya kupata chakula

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) leo limechapisha taarifa inayojulikana kama "taarifa ya utaratibu wa sanduku la vifaa" juu ya haki ya kupata chakula, mfumo ambao umekusudiwa kuzipatia nchi wanachama, taasisi za kimataifa, jumuiya za kiraia na wadau wengineo hati zinazofaa kutumiwa kutetea haki ya kupata chakula, haki ambayo ni sawa na haki za kimsingi za wanadamu.

Ofisa Mkuu Mtendaji wa Taasisi ya NEPAD azungumzia mwelekeo unaohitajika kusukuma mbele maendeleo Afrika

Mapema wiki hii, kabla ya kuzungumzia kikao cha Baraza Kuu la UM, kusailia ripoti kadha za KM, na kutoka wajumbe wa kimataifa na mashirika ya UM zilizozingatia huduma za kukuza maendeleo katika Afrika, Dktr Ibrahim Assane Mayaki, Ofisa Mkuu Mtendaji wa Taasisi ya Ushirikiano Mpya wa Maendeleo kwa Afrika (NEPAD), alifanya mahojiano maalumu na waandishi habari waliopo Makao Makuu.

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon amehuzunishwa na kifo cha Brigedia Jenerali Ahmed Moinuddin, Makamu Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi Amani vya UM katika Sudan Kusini (UNMIS), ambaye aliuawa Alkhamisi, mnamo tarehe 22 Oktoba, baada ya shambulio liliotukia Islamabad, Pakistan wakati akiwa mapumzikoni. KM alitumia salamu za pole ukoo wa wafiwa, wafanyakazi wa UNMIS na kwa Serikali ya Pakistan, na alitumai watu walioendeleza shambulio, watashikwa haraka na kufikishwa mahakamani.