Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO imechapisha mwongozo mpya kusaidia utetezi wa haki ya kupata chakula

FAO imechapisha mwongozo mpya kusaidia utetezi wa haki ya kupata chakula

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) leo limechapisha taarifa inayojulikana kama "taarifa ya utaratibu wa sanduku la vifaa" juu ya haki ya kupata chakula, mfumo ambao umekusudiwa kuzipatia nchi wanachama, taasisi za kimataifa, jumuiya za kiraia na wadau wengineo hati zinazofaa kutumiwa kutetea haki ya kupata chakula, haki ambayo ni sawa na haki za kimsingi za wanadamu.

Ripoti ya WFP imechapishwa katika wakati ambapo Mataifa kadha yanajaribu kushirikisha haki ya mtu kupata chakula kwenye sheria zao, na katika sera na miradi ya kitaifa. Mfumo wa FAO utatumiwa kama ni mwongozo wa kuwasaidia kuendesha kazi zao wale wabuni sera na wadau wanaohusika na utetezi wa haki za umma kupata chakula kinachoridhisha kuishi, hasa katika mazingira ya migogoro.