GAZA: Makaburi ya halaiki yaonesha waathirika walikuwa wamefungwa mikono - OHCHR
Ripoti za kutisha zinaendelea kuibuka kuhusu makaburi ya halaiki huko Gaza ambako waathirika wa Kipalestina wameripotiwa kuvuliwa nguo wakiwa wamefungwa mikono, jambo ambalo limezusha wasiwasi juu ya uwezekano wa kuweko kwa vitendo vya uhalifu wa kivita huku kukiwa na mashambulizi ya anga ya Israel yakiendelea kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR.