Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia waelimishwe ili waondokane na ajali za kuzama majini - Medard Wilfred

Medard Wilfred, Afisa Uhusiano  kwa umma katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, SAUT mkoani Mwanza nchini Tanzania akizungumza na Bosco Cosmas Vincent wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.
UN News

Masuala ya UM

Leo ni siku ya kimataifa ya kuzuia watu kuzama kwenye maji na siku hii imepatiwa kipaumbele na Umoja wa Mataifa kwa kutambua kwamba kila mwaka, takribani watu 236,000 hufa maji, na kufanya kuzama majini kuwa tatizo kubwa la afya ya umma duniani kote.  

Kuzama ni mojawapo ya sababu kuu za vifo duniani kwa watoto na vijana wenye umri wa kuanzia mwaka 1 hadi 24, kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa. Kuzama ni sababu ya 3 kuu ya kifo kitokanacho na majeraha bila kukusudia, ikichukua asilimia 7 ya vifo vyote vinavyohusiana na majeraha. 

Nchini Tanzania hususan Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, SAUT mkoani Mwanza, kaskazini magharibi mwa taifa hilo suala la wanafunzi kufa maji limekuwa ni hoja kwani wanafunzi watatu kwa nyakati tofauti walikufa maji kwa kuzama kwenye ziwa Victoria jirani na Chuo hicho. 

Je hatua gani wanachukua kuepusha suala hilo? Medard Wilfred, Afisa Uhusiano  kwa umma katika Chuo Kikuu hicho cha SAUT ambacho tayari kimepoteza wanafunzi kwa ajali za majini anaeleza zaidi katika video hii.