FAHAMU UMOJA WA MATAIFA
Je wafahamu Umoja wa Mataifa? Asili yake ni nini? Majukumu yake ni yapi? Ungana nasi!
Je wafahamu Umoja wa Mataifa? Asili yake ni nini? Majukumu yake ni yapi? Ungana nasi!
Kamishna mkuu wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Filippo Grandi amerejea kutoka nchini Syria na kutoa ombi jipya la kuongeza misaada ya kibinadamu, wakati mchakato wa rasimu ya katiba mpya ya Syria ukianza wiki hii.
Kutana na mkimbizi Fidaa kutoka Syria ambaye pamoja na familia yake walifungasha virago miaka minane iliyopita wakikimbia mapigano na kupata hifadhi Libya. Sasa changamoto za janga la corona au COVID-19 zimemlazimisha kurejea mapenzi ya zamani ya ufumaji ili kupata mkate wa kila siku wa familia yake.
Machafuko yanayoendelea kuongezeka kaskazini magharibi mwa nchi ya Syria yamesababisha vifo vya watoto na majeruhi kadhaa.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa misaada ya kibinadamu, OCHA, imeonesha wasiwasi wake kuwa ifikapo tarehe 10 mwezi huu wa Julai, kushindwa kuongeza idhini iliyowekwa na Baraza la Usalama la UN ya kuvusha misaada ya kibinadamu kutaongeza viwango vya mateso kwa raia ambavyo ambavyo havijaonekana katika kipindi cha miaka 10 ya mgogoro wa Syria.
Mkimbizi wa ndani Abbas Adu na wengine 400,000 wamelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula WFP kuwapatia msaada wa chakula wakati huu ambapo WFP imepaza sauti kwa wahisani kusaidia wananchi Milioni 41 wanaokabiliwa na njaa kutokana na hali mbaya ya hewa ambayo imeathiri mavuno yao na hivyo kukosa chakula.
Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto kwenye mizozo ya kivita Virginia Gamba amesema inasikitisha kuona ripoti ya mwaka kuhusu watoto na mizozo ya silaha inachapishwa katika kipindi ambacho bado kuna mateso makali kwa watoto katika maeneo mbalimbali ulimwenguni.
Takwimu za mpaka mwishoni mwa mwaka 2020 zilizotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi UNHCR zinaonesha duniani kote kuna jumla ya wakimbizi milioni 82.4.
Takwimu hizi huenda zikaongezeka mwaka huu kwa kuwa janga la Corona au COVID-19 limesababisha watu wengi kuyakimbia makazi yao.
“Baiyonuai inapungua, hewa ya ukaa inazidi kuongezeka, na uchafuzi wa hewa unaweza kuonekana kila sehemu kuanzia visiwani hadi milimani, ni lazima tufanye maamuzi ya kuwa na uhusiano mwema na mazingira yetu.”
Maafisa wakuu wa Umoja wa Mataifa leo wamelaani vikali shambulio baya lililofanyika katika hospitali nchini Syria mwishoni mwa wiki na kusisitiza haja ya uwajibikaji kwa uhalifu uliofanywa katika vita vya miaka kumi vya nchi hiyo.