Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Mkimbizi wa ndani nchini Msumbiji akipokea msaada wa chakula

Kuisaidia WFP ni kuwasaidia wakimbizi kama Adu

© WFP/Grant Lee Neuenburg
Mkimbizi wa ndani nchini Msumbiji akipokea msaada wa chakula

Kuisaidia WFP ni kuwasaidia wakimbizi kama Adu

Msaada wa Kibinadamu

Mkimbizi wa ndani Abbas Adu na wengine 400,000 wamelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula WFP kuwapatia msaada wa chakula wakati huu ambapo WFP imepaza sauti kwa wahisani kusaidia wananchi Milioni 41 wanaokabiliwa na njaa kutokana na hali mbaya ya hewa ambayo imeathiri mavuno yao na hivyo kukosa chakula.

 
“Familia yangu ina wasiwasi na Mabadikilo ya hali ya hewa, Mwaka jana hali ilikuwa nzuri na tulipata mavuno mazuri.”  
 
Ni maneno ya Kijana Abbas Adu, mzaliwa wa Chad katika kijiji cha Fatima, lakini sasa yeye pamoja na wanavijiji wengine zaidi ya laki 4 wanaishi karibu na Mto CHAD. 
 
Abbas anasema “Lakini Mwaka huu hali si nzuri na mvua imechelewa sana, tumeteseka sana. Tuna njaa, hali ya hewa ni mbaya sana, ikiwa hakuna mvua, hakutakuwa na nyasi wala miti, na watu wengi wanakufa sababu ya hali mbaya ya hewa.”  
 
Kilio chao kinajibiwa na WFP ambayo magari yake yanaasilisha msaada wa chakula na maisha ya kina Abbas sasa yanapata nuru . 
 
Pamoja na changamoto, Adu ana ndoto yakuwa Afisa Misitu au kufanya kazi idara ya maji ili aweze kusaidia wanajamii kupata uhakika wa chakula na samaki.  
 
Ingawa ni mwanafunzi na mcheza mpira maarufu eneo hilo lakini pia ni mvuvi akisema, “Kuvua samaki na shughuli za shamba ni ngumu sana, lakini ndio njia pekee yakutuwezesha kupata chakula” 
 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa WFP watu milioni 41 wanakabiliwa na baa la njaa ambapo wanahitaji msaada wa Dola za Kimarekani Bilioni 6 ili kuweza kuwasaidia wakimbizi wa ndani na nje na wametoa angalizo dunia isisubiri kuanza ikitangaziwa idadi ya vifo ndio ikaanza kusaidia.