Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto watatu wauawa nchini Syria:UNICEF

Magari yaliyobeba misaada yakiwa kwenye foleni katika mpaka wa Uturuki kuingia Syria
OCHA/David Swanson
Magari yaliyobeba misaada yakiwa kwenye foleni katika mpaka wa Uturuki kuingia Syria

Watoto watatu wauawa nchini Syria:UNICEF

Amani na Usalama

Machafuko yanayoendelea kuongezeka kaskazini magharibi mwa nchi ya Syria yamesababisha vifo vya watoto na majeruhi kadhaa. 

Taarifa iliyotolewa leo na mkurugenzi mkuu wa kanda ya Mashariki ya kati na Afrika magharibi – MENA Ted Chaiban imesema wamethibitisha baadhi ya vifo. 

UNICEF imethibitisha leo asubuhi, watoto watatu wameuawa katika mashambulizi mawili tofauti katika eneo hilo. Mashambulizi yametokea katika eneo ambako machafuko yamepungua licha ya kusitishwa mapigano toka mwezi Machi mwaka jana” 

Chaiban ameongeza kuwa Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, imethibitishwa takribani Watoto 10 wameuawa nchini Syria.
“Hii ni ishara mbaya kuwa mapigano yanarudi tena Syria. Jamii zipo kwenye hatari kubwa yakupoteza mapumziko kidogo ya machafuko waliyokuwa nayo wakati wa utulivu wa vurugu.” 

Ameeleza kuibuka tena kwa ghasia na mapigano kutawaweka mbali watu wa Syria mbali na kufikiwa amani na suluhu ya kisiasa ambayo inalenga kumaliza umwagaji damu na kutatua mzozo uliodumu kwa zaidi ya muongo mmoja.