Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAHAMU UMOJA WA MATAIFA

Bendera za nchi wanachama wa UN
UN /Rick Bajornas
Bendera za nchi wanachama wa UN

FAHAMU UMOJA WA MATAIFA

Masuala ya UM

Je wafahamu Umoja wa Mataifa? Asili  yake ni nini? Majukumu yake ni yapi? Ungana nasi!

Mabaki ya jengo huko Hiroshima nchini Japan baada ya kuangushwa kwa bomu la atomiki. Majengo yalisalia magofu.
UN /DB
Mabaki ya jengo huko Hiroshima nchini Japan baada ya kuangushwa kwa bomu la atomiki. Majengo yalisalia magofu.

Mnamo mwaka 1945, mataifa yalikuwa magofu. Vita vya pili vya dunia  vilikwisha na ulimwengu ulihitaji amani.

Mataifa 51 yalikusanyika huko San Francisco mwaka 1945  kutia saini hati ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa

Utiaji saini wa Katiba au Chata ya UN tarehe 26 mwezi Juni mwaka 1945  kwenye jengo la maveterani huko San Fransisco, Marekani.
UN/Youd
Utiaji saini wa Katiba au Chata ya UN tarehe 26 mwezi Juni mwaka 1945 kwenye jengo la maveterani huko San Fransisco, Marekani.

Hati hii ilikuwa ni mkataba, ukiunda shirika jipya ambalo si jingine bali ni Umoja wa Mataifa.

Miaka 70 baadaye, Umoja wa Mataifa unadumisha amani na usalama wa kimataifa.

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wakikarabati barabara muhimu za usambazaji huduma za kibinadamu Sudan Kusini
UN/Isaac Billy
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wakikarabati barabara muhimu za usambazaji huduma za kibinadamu Sudan Kusini

Umoja wa Mataifa unakuza maendeleo na kupatia wahitaji misaada ya kibinadamu.

Umoja wa Mataifa unatetea sheria ya kimataifa, unalinda haki za binadamu, na kukuza demokrasia.

Taswira ya angani ya bonde la Msimbazi jijini Dar es salaam nchini Tanzania ambako mafuriko  ya mapema mwaka  huu yalisababisha vifo vya watu wapatao 15. Hivi sasa Benki ya Dunia na serikali ya Tanzania zimeibuka na mbinu ya kuboresha eneo hilo.
Benki ya Dunia/Screenshot
Taswira ya angani ya bonde la Msimbazi jijini Dar es salaam nchini Tanzania ambako mafuriko ya mapema mwaka huu yalisababisha vifo vya watu wapatao 15. Hivi sasa Benki ya Dunia na serikali ya Tanzania zimeibuka na mbinu ya kuboresha eneo hilo.

Na kwa sasa, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zinafanya kazi pamoja kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Umoja wa mataifa unasaidia kujenga ulimwengu bora kama vile ambavyo waanzilishi wake walivyotamani miaka 70 iliyopita.

Maelezo ya Jumla

Ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifajijini New York Marekani
UN/Eskinder Debebe
Ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifajijini New York Marekani

Umoja wa Mataifa ni shirika la kimataifa lililoanzishwa mwaka 1945.  Hivi sasa lina mataifa wanachama 193. Utendaji na kazi za Umoja wa Mataifa huongozwa na malengo na kanuni zilizomo kwenye mkataba wake anzilishi.

Mataifa Wanachama

Kila nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa ni mjumbe wa Baraza Kuu.  Mataifa yanakubaliwa kuwa wanachama wa UM kwa uamuzi wa Baraza Kuu baada ya kupendekezwa na Baraza la Usalama.

Vyombo Vikuu

Wajumbe wa Baraza la  Usalama kikaoni 19 Februari 2019
UN/Eskinder Debebe
Wajumbe wa Baraza la Usalama kikaoni 19 Februari 2019

Vyombo vikuu vya vya Umoja wa Mataifa ni Baraza Kuu, Baraza la Usalama, Baraza la Uchumi na Jamii, Baraza la Udhamini, Mahakama ya Kimataifa ya Haki na Sekretarieti. Vyote hivi viliundwa mwaka 1945 wakati Umoja wa Mataifa ulianzishwa.

Uongozi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni alama ya maadili ya shirika na msemaji mkuu wa shirika kwa maslahi ya watu wa ulimwenguni, hususan maskini na wale walio hatarini zaidi kudhuriwa. Katibu Mkuu wa sasa wa Umoja wa Mataifa, na ambaye ni wa 9 kushika wa waadhifa huu ni Bwana António Guterres kutoka Ureno. Alichukua mamlaka mnamo Januari 1, 2017. Mkataba wa UM humweleza Katibu Mkuu kama ‘Ofisa Mkuu Tawala’ wa shirika.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
TASS/ UN DPI
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres

Sekretariati

Sekretarieti, mojawapo wa kiungo muhimu cha Umoja wa Mataifa, imepangiliwa kwa misingi ya idara, kila idara au ofisi ikiwa na eneo la utendaji na jukumu dhahiri. Ofisi na idara huratibiana kuhakikisha kuna uwiano zinapotekeleza kazi za kila siku za shirika katika ofisi na vituo vya kazi kote duniani. Kiongozi wa Sekretarieti ya Umaja wa Mataifa ni Katibu Mkuu.

Fedha, Programu, Mashirika Maalumu na Mengine

Mfumo wa Umoja wa Mataifa, UMM, unaojulikana rasmi kama ‘‘familia ya UM’’umeundwa na Umoja wa Mataifa wenyewe na programu zingine zinazohusiana, fedha na mashirika maalumu zote zikiwa na uanachama wao, uongozi na bajeti. Programu na fedha hufadhiliwa kwa njia ya kujitolea kinyume na michango kadiriwa. Mashirika Maalumu na mashirika huru ya kimataifa yanafadhiliwa kwa njia ya kujitolea na michango iliyokadiriwa

ASILI NA HISTORIA

Jina ‘‘Umoja wa Mataifa’’, lililobuniwa na Rais wa Marekani Franklin D. Roosevelt, lilitumika kwanza katika tangazo la ‘‘Umoja wa Mataifa’’ la Januari 1, 1942 wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Dibaji ya Katiba ya Umoja wa Mataifa (ikiwa kwa lugha ya kichina) ikielezea misingi na malengo ya watu wote ambao serikali zao zimeridhia kuanzisha Umoja wa Mataifa.
UN/McCreary
Dibaji ya Katiba ya Umoja wa Mataifa (ikiwa kwa lugha ya kichina) ikielezea misingi na malengo ya watu wote ambao serikali zao zimeridhia kuanzisha Umoja wa Mataifa.

HATI MUHIMU

Mkataba wa wa Umoja wa Mataifa

Tamko la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa

Nakala za awali za tamko la haki za bindamu.
UN Picha/Greg Kinch
Nakala za awali za tamko la haki za bindamu.

Mkataba ulioanzisha Mahakama ya Kimataifa ya Haki